Thursday, February 6, 2014

UKATILI WA KUTISHA!! MWANAMKE AMWAGIWA MAFUTA YA MOTO NA MAMA MWENYE NYUMBA HUKO GEITA

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Pendo Ladislaus (28)mkazi wa mtaa wa Lwenge wilayani Geita amemwagiwa mafuta ya moto na kuunguzwa vibaya sehemu za kifuani na tumboni baada kuhitirafiana na mama mwenye nyumba alipopanga aitwaye Bi Leticia Charles.

Tukio hilo limetokea Januari 31 mwaka huu majira ya saa kumi jioni.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Geita Dk Adam Sijaona amethibitisha kumpokea mama huyo na amelazwa wodi namba saba na hali yake inaendelea  vizuri.

 Na Valence Robert-Geita

No comments:

Post a Comment