WAZAZI na walezi mkoani Shinyanga wameaswa kuacha tabia ya
kuwatelekeza watoto wao katika kituo maalumu cha kulea watoto
wenye ulemavu wa ngozi (Albino)wasioona na wenye ulemavu wa kusikia
Buhangija manispaa ya Shinyanga,kutokana na kukua bila kuwafahamu wazazi , wala kuelewa walizaliwa
wapi nakushindwa wakati wa rikizo kwenda nyumbani.
Akizungumza mara baada ya kutembelea kituo hicho jana
Anna Mwalongo na familia yake, kwa lengo la kutoa msaada wa chakula cha pasaka
kwa watoto hao pamoja na kambi ya wazee wakoma Kilandoto,alisema inasikitisha
kuona wazazi hawana uchungu na watoto wao na kukaa bila kuwakumbuka kuwajulia
hali na maendeleo yao.
Anna Mwalongo ambaye pia ni muuguzi katika hospitali ya mkoa
wa Shinyanga ,alisema ameamua kutoa msaada wa kilo 100 za mchele,mafuta lita 20
na mbuzi wanne kwa vituo vyote viwili kwa kushirikiana na familia yake,ili
kuwawezesha watoto hao na wazee
kusherehekea sikukuu ya kufufuka yesu kristo kama watu wengine badala ya kujiona
kama wametengwa na jamii.
" inasikitisha mtoto kutomjua mama yake na wala kufahamu sehemu aliyozaliwa hata wakati
wa rikizo kuendelea kuishi katika eneo hili la kituoni,kutokana na imani iliyojengeka akirudi katika familia atauwawa, nawaomba
wazazi wenzangu tuwakumbuke watoto wetu hata kuwatembelea ni faraja kubwa “mama
Mwalongo.
Mlezi wa kituo hicho
Maisala Adinani alisema kuwa , baadhi ya
wazazi na walezi wamekuwa wakishindwa kufika kuwaona watoto wao ambapo wengine
tangu waletwe imefika miaka saba
hawajawahi kuwaona wazazi wao ama kuwatembelea na kuwajulia hali.
Nao baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi hamis hassan na Limi Juma waliwataka wazazi
kuona umuhimu wa kurudi kuwatembelea kituoni,nasiyo kuwaacha miaka yote bila
kuwakumbuka kitendo ambacho ni kuwatelekeza na kuachia jukumu hilo serikali
huku wao wakisahau kabisa kama wanawatoto albino.
“Inatuuma sana inapofika muda wa kufunga shule sisi tunabaki
kituoni watoto wengine wanachukuliwa na ndugu zao,hata sisi tunatamani kuwaona
wazazi wetu tatizo hawajarudi tena kituoni tangu tufike ila tunamshukuru mungu
kwa kuwa tunapata wageni wengi wanatutembelea na kutufariji pamoja na kutupa
msaada”alisema Hassan.
Naye afisa ustawi wa jamii msaidizi wa kambi ya wazee wakoma Kolandoto Evodia Ndaka,alisema jamii haina budi kuiga
mfano huo wa kukumbuka makundi maalumu katika jamii,kwani wanahitaji msaada
zaidi kwakuwa ni wazee hawana uwezo wa kupata kipato hivyo jukumu linakuwa kwa
serikali na jamii nzima.
Naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga David
Nkulila,alisema ni vema watu wakawa na upendo kwa kuwasaidia watoto na wazee
pamoja na wasiojiweza,badala ya kuiachia serikali kwa kila jambo huku
akipongeza hatua ya kutoa msaada wa chakula na mbuzi kutoka kwa familia ya
Josephat Mwalongo na kuitaka jamii nzima kuiga mfano huo.
Zaidi ya miaka sita imepita
tangu kuanza kwa mauaji ya albino
mwaka 2007,ambapo taifa limepata doa kubwa na watu wenye ulemavu wa
ngozi takribani 72 walipoteza maisha, watu 28
walijeruhiwa 19 walifukuliwa wakiwa
wamezikwa.
No comments:
Post a Comment