MILA na desturi zilizopitwa na wakati bado ni changamoto
kubwa katika mkoa wa Shinyanga kutokana na baadhi ya wananchi hasa jamii ya
wafugaji, kuhifadhi fedha zao kwenye mazizi ya ngombe kwa kuchimbia ardhini
hali ambayo inadhorotesha uchumi wanchi kukua na kuendelea kuwa masikini.
Hayo yalielezwa hivi
karibuni na meneja wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui wakati
akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa habari kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi
wa hotel ya Diamond Fields mjini Shinyanga.
Meneja Pamui ambaye alikuwa mgeni rasmi , aliwataka
waandishi kuendelea kuandika habari za kuelimisha jamii ili ijenge
utamaduni wa kutunza fedha zao kwenye
taasisi za fedha, badala ya kuweka ndani
au kwenye mazizi ya ngombe huku akibainisha kuwa njia hizo siyo salama pia
zinadidimiza uchumi wa nchi kutokana na fedha kutozunguka.
“Andikeni kwa kufichua maovu lakini pia na mazuri yaliyopo
myaripoti jamii ijuwe,katika mikoa ya
kanda ya ziwa wananchi wengi hawana mwamko wa kuhifadhi fedha zao benki ,hii
changamoto nyinyi wanahabari mnapaswa kutusaidia kutoa elimu kupitia vyombo
vyenu mnavyofanyia kazi “alisema Pamuye.
Katika hatua nyingine meneja huyo alichangia rimu 50 za
karatasi kwenye stationary ya klabu ya
waandishi wa habari ,ambapo aliwataka
wadau wengine kuunga mkono juhudi zinazofanywa na waandishi kuutangaza mkoa huo
kwa kuripoti mara kwa mara matukio na shughuli nyingine za maendelo.
Naye mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga (SPC) Shija Felician, aliwataka wadau kuendelea kutoa ushirikiano kwa
vyombo vya habari wakati wa kufuatilia matukio huku hakusita kuzinyoshea kidole
baadhi ya halmashauri, ambazo bado zina urasmu wa kutoa habari jambo ambalo
linaminya uhuru wa kupata habari.
Alisema bado vitendo
vya kuminya uhuru wa wanahabari vinaendelea kutokea sehemu mbalimbali hapa
nchini ,ikiwa ni pamoja na kunyanyaswa kwa kupigwa ,kuharibiwa vifaa vya kazi
na ushirikiano mdogo kwa baadhi ya viongozi hasa wa serikali na kuwataka
wandishi kutokata taama bali waongeze bidii.
Kwa upande wake mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa
Shinyanga(RCO) Husein Kashindye ,alisema sekta ya habari ni muhimu kwa kuwa
wanafikisha ujumbe sehemu kubwa kwa wakati mmoja,ambapo nguvu hiyo ikitumika
kuelimisha jamiii kuachana na imani potofu za kuwa vikonge kwani nao wanahaki
ya kuishi.
No comments:
Post a Comment