WAKULIMA wa mpunga 860 wa kijiji cha Itilima wilaya ya
Kishapu mkoa wa Shinyanga wameshindwa kunufaika na mradi wa umwagiliaji uliojengwa kwa ajili ya kilimo cha mpunga,
kutokana na kukosa chanzo cha maji ya uhakika na mradi kutelekezwa kugeuka kuwa
sehemu ya kichaka cha wanyama huku million 302 zilizotumika zikiteketea bila
mafanikio.
Hali hiyo ilibainika jana wakati wa ziara ya Naibu waziri wa
kilimo chakula na ushirika Godfrey Zambi
,mara baada ya kutembelea eneo la mradi na kukutana na adhaa ya kukosa njia ya kuelekea mradi ulipo hivyo
kulazimika kukatisha kwenye kichaka cha majani hali ambayo ilimpa wakati mgumu
kutokana na mazingira yalivyokuwa.
Kutokana na hali hiyo,Naibu waziri alimuagiza mkuu wa wilaya
hiyo Wilson Nkhambaku kuhakikisha eneo la mradi linafanyiwa usafi hata kama
haufanyi kazi,huku akionyesha kusikitishwa jinsi fedha za walipa kodi
zinavyoteketea kwa kuwekeza miradi ambayo haina tija kwa wananchi na viongozi
waeneo husika wakishindwa kuisimamia.
“Hii hali inadhihirisha wazi hapa wataalamu hawatembelei
miradi ,mnautelekeza mpaka eneo limekuwa msitu hivi kweli wilaya imeshindwa
kusimamia mradi ukawa katika hali nzuri inaniuma sana,hapa mfano akitokea
mfadhili aliyetoa fedha zake anaweza kutoa machozi jinsi hali ilivyo
mbaya”alisema Zambi.
Naibu waziri Zambi aliwataka wataamu wa umwagiliaji kutoa
ushauri mzuri kabla ya kujenga miradi hatua itakayosaidia kuokoa fedha za umma
ambazo zimekuwa zikitumika vibaya kwa kujenga miradi isiyo na tija kwa wakulima
hivyo kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuiacha kuwa vichaka licha ya
kutumia fedha nyingi.
Akiwa wilayani humo alitembelea kijiji cha Nyenze ili kuona mradi wa
umwagiliaji lakini hali ilikuwa tofauti baada ya kukuta eneo la hekta 450 lililotengwa hakuna shughuli iliyofanyika,
hivyo kuishia kuangalia eneo la mbuga kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji huku
wataalamu wakivutana baadhi wakipendekeza kujengwa bwawa na wengine mifereji
ambapo fedha iliyotengwa ni million 298 kutoka TAMISEMI).
Awali mkuu wa wilaya hiyo Wilson Nkhambaku akitoa taarifa
kwa Naibu waziri, alisema mradi huo
ambao ulikamilika mwaka 2005 ,ulilenga kuwanufaisha wakulima lakini
kutokana na mkondo wa mto Mumbu kuhama lengo limeshindwa kufikia ambapo shemu
lililpjengwa banio kingo zake sio imara na ina mtelemko wa taratibu.
Naye mwenyekiti wa umoja wa watumiaji maji Dominic Philipo
alisema kwa sasa wananchi wa kijiji hicho hawapati chakula cha kutosha kutokana
nakushindwa kulima kilimo cha umwagiliaji na kuitaka serikali kuangalia
uwezekano wa kuwasaidia ili waondokane na tatizo hilo,kwani awali mradi
ulipokuwa unafanya kazi mazao yalistawi kwa kuwa na maji ya uhakika lakini sasa
wamekwama kuendelea kulima na kusubili mvua za masika pekee.
No comments:
Post a Comment