UTOAJI wa zabuni kwa njia za kinyemela umesababisha baadhi
ya miradi ya umwagiliaji kushindwa kutekelezeka
huku serikali ipoteza mamilion ya fedha kugharamia miradi hiyo,
na kuwaacha wananchi wakiwa hawana matumaini ya kumalizika kero hiyo
ili waweze kuendesha shughuli za kilimo .
Kauli hiyo ilitolewa Naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika
Godfrey Zambi mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa bwawa ,katika kijiji
cha Ishololo halmashauri ya Shinyanga na kukelwa na shughuli iliyofanywa na
kampuni ya Syscon Builders JV Marcotech Co Ltd ya jijini Dar es salaam .
Kampuni hiyo iliingia mkataba Februari 15 ,2013 kwa jumla ya
sh 940.3 milion na wizara hiyo baada ya
kushinda zabuni ,ambapo kwa sasa mradi huo umesimama kutokana na uwezo mdogo wa
kifedha vifaa na kwamba ulitakiwa kukamilika 15 Dec 2013 huku vifaa vyote vya
kazi vikiwa vimeharibika na kuachwa eneo la mradi.
Akiwa eneo la mradi huo Naibu waziri Zambi alisema serikali
ilidhamilia kuanzisha mradi lakini mkandarasi amekuwa tatizo na hiyo inatokana
na kupewa zabuni kinyemela kwani hana sifa ya kufanya kazi hiyo zaidi ya
kupoteza fedha za wananchi na kuahidi kufuatilia suala hilo ili wananchi wapate
bwawa.
“Nakiri wazi wizara yangu ndiyo ilifunga mkataba huu na hapa
siwafichi suala hili nitalifuatilia mpaka hatua ya mwisho haiwezekani fedha za
wananchi zichezewe chezewe tu,mradi umenisikitisha sana kazi iliyofanyika ni ya
hovyo na tayari milon 200 zimeshatumika ,nitakaa na wataalamu wa wizara tuone
cha kufanya”alisema Zambi.
Injinia wa skimu ya umwagiliaji wa halmashauri hiyo Godfrey Mbwambo alisema kuwa mradi huo ulilenga kuwanufaisha wakulima
na wafugaji kutoka vijiji viwili
vya Ishololo na Tindeng’hulu, ambao ungeweza kunufaisha wakulima
zaidi ya 1500 na kiasi cha hekta
zipatazo 500 kwa kumwagiliwa maji kutoka katika bwawa hilo.
“Mradi huu unafadhiliwa
na mradi wa uwekezaji katika sekta
ya kilimo wilaya (DASIP) ambayo ilichangia kiasi cha zaidi ya shilingi millioni 740 na mfuko wa umwagiliaji (DIDF) kwenye
mradi huo umechangia shi millioni 200 na kufanya jumla ya gharama ya mradi
ya shilingi millioni 940.3”alisema
Mbwambo.
Naye mbunge viti
maalum Azzah Hilali alisema wao
halmashauri na kata hawana maelezo ya mradi huo kwa kuwa uko chini ya wizara na
kumtaka mhandisi umwagiliaji kanda ya ziwa Ebenezer Kombe kutoa maelezo ya
kina, kwani ndiyo wasimamizi pamoja na wizara
huku akiweka wazi kuwa wakulima
wamekuwa wakilalamika kushindwa kutekelezeka kwa wakati na kukwamisha
shughuli za kilimo.
Mhandisi wa umwagiliaji ofisi ya kanda ya ziwa Ebenezer
Kombe alikiri wazi kuwa utekelezaji wake hauridhishi na kuahidi kuendelea kusimamia ili kuweza
kuwasaidia wananchi kupata huduma ya bwawa na kuendesha shughuli za kilimo cha
umwagiliaji.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Mohamed Kiyungi alimuomba Naibu waziri
kiasi cha sh 200 milion zilizotoka DIDF na kuhamishiwa akaunti ya mradi wa DASIP
Mwanza , zirudishwe kwenye akaunti ya halmashauri ili ziweze kuendeleza shughuli
za miradi ya umwagiliaji.
Diwani wa kata ya Usule eneo ulipo mradi huo Amina Bundala
alisema kazi hiyo ilitakiwa ifanyike
ndani ya siku 240 sawa na miezi nane
,licha ya kuongezewa muda lakini imeshindikana na kufanya wao waonekane
waongo kutokana na majibu kwa wananchi
na kupelekea mifugo kunywa matope badala
ya maji na mashamba ya wakulima
kuvurugwa mashamba yao.
Mradi huu uliibuliwa na wananchi wenyewe katika bajeti ya
kijiji ya mwaka 2011/12 kwa kutaka bwawa kwaajili ya kilimo cha
umwagiliaji kwa zao la mpunga ikiwa walikuwa wakikosa maji ya kutosha kwa
kuliendeleza zao hilo na kupata mavuno
ya kutosha huku halmashauri ikipata pato la ndani zaidi kupitia
ushuru za zao la mpunga.
No comments:
Post a Comment