Monday, June 23, 2014

MAKUBWA YAIBUKA KIKAO CHA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA, NI BAADA YA WAKAGUZI WA NDANI KUBAINI UMRI WA KUZALIWA WA BAADHI YA WATUMISHI NI ZAIDI YA MIAKA 100.

Baadhi ya madiwani wakiwa kwenye kikao cha dharura cha baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga kilichoketi kujadili kanuni za uendeshaji wa halmashauri hiyo pamoja na taarifa ya kamati ya fedha.

Naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila akifungua kikao cha dharura cha baraza la madiwani katika ukumbi wa makao makuu ya ofisi ya mkuu wa mkoa huo,ambapo aliwataka kuhakikisha wanaweka itikadi za vyama vyao pembeni ili kujadili maendeleo ya manispaa yao.

Madiwani wakiendelea kufuatilia maelekezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na kiongozi wao.

Kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga Projestus Lubanzibwa akizungumza na madiwani,ambapo aliwaasa kujadili kwa kina taarifa zilizotolewa,huku akiwasisitiza watalaamu wa manispaa kutoa majibu ambayo hayataacha maswali kwa wananchi  na madiwani katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.



Nimadiwani wakiendelea kufuatilia ukurasa kwa ukurasa taarifa iliyotolewa na mkaguzi wa ndani wa manispaa hiyo Mussa Sylvester,ambayo ilidai kuwa baadhi ya watumishi taarifa za umri wao wa kuzaliwa zinatofautiana,huku kwenye mafaili na mfumo wa computer zikionyesha baadhi yao wanazaidi ya miaka 100.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi akizungumza kwenye kikao hicho,alisema mwakani utafanyika uchaguzi mkuu hivyo ni vyema ukumbi wa mikutano wa manispaa hiyo uliochomwa moto wakati wa uchaguzi uliopita ukafanyiwa usafi kuliko hali iliyopo sasa kwani inatisha kutokana na jinsi lilivyoteketea.

Madiwani wanashauriana nini kifanyike kutokana na changamoto zilizopo kwenye manispaa yao.

Kikao bado kinaendelea tunasikiliza kwa makini.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Festo Kangombe,akijibu hoja za madiwani ambao walihoji kukosekana kwa mwanasheria wa manispaa hiyo,alidai kuwa tayari taratibu zimekamilika na kwamba muda si mrefu watapata hatua itakayosaidia kuondoa usumbufu wa ucheleweshaji wa kesi kusikilizwa.

Madiwani na wataalamu wa manispaa ya Shinyanga wakipitia taarifa zilizowasilishwa kwenye kikako cha dharura cha baraza la madiwani.



No comments:

Post a Comment