MKAZI mmoja wa kijiji cha Masuguru
kata ya Mwaduiluhumbo wilaya ya Kishapu aliyefahamika kwa jina la Juma Masalu
(25) , ameuawa kwa kupigwa risasi baada
ya kuvamia ndani ya mgodi wa madini ya Almasi, unaomilikiwa na kampuni
Wiliamson Diamond akiwa na wenzake 20 kwa lengo la kuiba mchanga unaosadikiwa
kuwa na madini.
Tukio hilo lilitokea
Juni 13 mwaka huu majira ya saa 5:00 usiku kufuatia kundi hilo kuvamia mgodi
wakiwa na silaha za jadi mishale,mikumi,makombeo ya kurusha,ndipo walinzi wa
kampuni ya Zenith wanaolinda mgodi huo walijihami kwa kupiga risasi za moto na
kusababisha mauaji hayo na mmoja kujeruhiwa mguuni huku wengine wakikimbia.
Matukio ya uvamizi kama
huo yanayofanywa na vijana wanaojiita wabeshi yamekuwa yakitokea mara kwa mara
,ambapo mwaka jana kundi la watu zaidi ya 100 walivamia mgodi huo wakiwa na
silaha za jadi wakitaka kuchukua mchanga wa almasi na kusababisha wawili
kujeruhiwa na kupata ulemavu wa maisha baada ya kukatwa miguu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
jana kwa vyombo vya habari na kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani shinyanga
, Kihenya Kihenya alisema walinzi walianza kupambana nao kwa kuwa rushia risasi,
huku wavamizi hao wakirusha silaha za jadi walizoingia nazo na baadaya
kuzidiwa nguvu walikimbia na mwenzao
kupoteza maisha papo hapo aiyepigwa risasi sehemu za siri.
Kaimu kamanda alimtaja aliyejeruhiwa
kwa risasi kuwa ni Emmanuel Charles (23) mkazi wa kata ya majimaji mji wa
maganzo,ambaye alipigwa risasi mguu wa kushoto kisha kukamatwa na kupelekwa katika zahanati ya Mgodi huo kwa
kupatiwa matibabu huku akishikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.
Kufuatia tukio hilo la mauaji
kutokea walinzi wawili wa kampuni ya Zenith ambo majina yao hayafahamika, waliokuwa
wakipambana na wavamizi hao wanaofahamika kwa jina la Wabeshi walikimbia kusiko julikana wakihofia kukamatwa na kuzitelekeza bunduki zao.
Jeshi la polisi mkoani humo
linawatafuta wavamizi wengine kumi na nane waliokimbia mara baada ya kuzidiwa kwa mashambulizi ya silaha za moto iliwaweze
kutiwa nguvuni na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuwataka vijana
kutafuta shughuli zingine na siyo kuvamia mgodi kutafuta madini.
Matukio ya uvamizi kama
huo yanayofanywa na vijana wanaojiita wabeshi yamekuwa yakitokea mara kwa mara
,ambapo mwaka jana kundi la watu zaidi ya 100 walivamia mgodi huo wakiwa na
silaha za jadi wakitaka kuchukua mchanga wa almasi na kusababisha wawili
kujeruhiwa kwa risasi na kupata ulemavu
wa maisha.
No comments:
Post a Comment