Thursday, June 5, 2014

KAMPUNI YA BARRICK YAWAKIVUTIO SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI SHINYANGA ,MAMIA YA WANANCHI WAFURIKA KUJIONEA BIDHAA MBALIMBALI KWENYE BANDA LAO.


Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselm Tarimo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Shilabela wilaya ya Shinyanga mara baada ya kukagua mabanda kwa ajili ya maonesho katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambayo yamefanyika kimkoa kijijini humo.
Katika hotuba yake katibu tawala aliipongeza kampuni ya African Barrick gold kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendelea kuhifadhi mazingira na kuitaka jamii nzima kujenga utamaduni wa kupanda miti katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuhifadhi vyanzo vya maji.

Afisa mahusiano ya jamii mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo  akimkabidhi mche wa mti wa matunda katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi,kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kimkoa kijiji cha Shilabela.



Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza wakiwa katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani.

Afisa mahusiano ya jamii mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akifafanua jambo juu ya uhifadhi wa mazingira na umuhimu wa kupanda miti.







Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselm Tarimo aliyevaa suti akielekea kukagua mabanda ya maonyesho bidhaa mbalimbali katika siku ya mazingira duniani kijiji cha Shilabela wilaya ya Shinyanga.kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku na kulia ni katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi.

Afisa uhusiano wa mgodi wa Buzwagi Moses Msofe akifafanua  huduma wanazozitoa kwa kwa jamii,ambapo alisema wanaelimisha jamii umuhimu wa kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti na kutunza vyanzo vya maji.

Afisa afya wa mkoa wa Shinyanga Neema Simba akipokea zawadi kwa niaba ya Paul Kadonya ambaye ni mshindi wa tuzo ya rais ngazi ya kaya kutoka kijiji cha Nyandekwa wilaya ya kahama ambaye hakuhudhuria maadhimisho hayo.

Jeshi la jadi sungusungu la kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza wakitoa burudani kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani .

Afisa mazingira mgodi wa Buzwagi Tunzo  Msuya akitoa maelezo kwa mgeni rasmi katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Tarimo ,kuwa wanatoa miche ya miti ya matunda kwa jamii na miti mbalimbali ili kuhifadhi mazingira na kutunza uoto wa asili.

Afisa maliasili na mazingira mkoa wa Shinyanga Bilie Edimott akitoa taarifa ya washindi wa tuzo ya rais katika kuhifadhi mazingira ,ambapo wilaya iliyoongoza ni Kahama na upande wa migodi ni Barrick na mgodi wa almas wa mwadui katika wilaya ya Kishapu.

Afisa mazingira wa mgodi wa Buzwagi Naziel Eliakimu akitoa ufafanuzi kwa wananchi jinsi mgodi huu unavyofanyakazi katika kuhifadhi mazingira,wanyama na mimea na namna ya kukabiliana na changamoto za uhifadhi mazingira.









 









No comments:

Post a Comment