Tuesday, June 3, 2014

VIFO VYA MAMA NA MTOTO CHINI YA MIAKA MITANO SHINYANGA VYA WASHITUA WADAU WAKUTANA KUPANGA MIKAKATI YA KUMALIZA TATIZO HILO.

Wadau wakisikiliza kwa makini maelekezo yanayotolewa na wataalamu katika kuboresha huduma za afya na kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto mkoa wa Shinyanga.


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizungumza na wadau kwenye warsha ya kujadili jinsi ya kupunguza vifo vya mama na mtoto kwenye mkoa huo na kuhakikisha zinaboreshwa katika vituo vyote na zahanati.
Aliwataka wadau hao kuzingatia maazimio 11 waliojipangia ili kuboresha huduma za afya mijini na vijijini sanjari na kutoa elimu kwa jamii hasa waishio pembezoni ambao wamesahaulika bila ya kufanya hivyo jitihada na mikakati yao itaishia kuandikwa kwenye makaratasi .


Baadhi ya wadau wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika warsha ya siku moja ya kujadili namna ya kupunguza vifo vya mama na mtoto chini ya miaka mitano katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo.

Mwakilishi msaidizi kutoka UNFPA Rutasha Dadi akifafanua jambo juu ya mikakati iliyowekwa ya kupunguza vifo vya mama na mtoto chini ya miaka mitano wakati wa warsha iliyofanyika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.


Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Ntuli Kapologwe akiwasilisha taarifa ya hali ya afya ya uzazi mkoani humo,ambapo alisema hali ni mbaya kutokana na idadi ya wanawake wanaopoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi kuongezeka tofauti na ilivyokuwa mwaka 2012.
Dkt. Kapologwe alisema mwaka 2012 vifo vilivyotokana na matatizo ya uzazi vilikuwa 46 lakini mwaka 2013 idadi iliongezeka na kufikia 61 na kutaja sababu ni uwajibikaji mdogo wa watumishi,jamii kutokuona mwamko wa kujifungulia vituo vya afya na umbali wa huduma za afya jambo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi haraka.






Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu Isabela Chilumba akichangia mada kwenye warsha ya wadau katika kupunguza vifo vya mama na mtoto mkoa wa Shinyanga,ambapo alisema katika halmashauri yake tayari wameanza kutekeleza kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii umuhimu wa kwenda hospitali.

  












No comments:

Post a Comment