Thursday, June 26, 2014

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC YAWATAKA WATANZANIA KUTOOGOPA MABADILIKO YA KUTUMIA MFUMO WA BIOMETRIC VOTER REGISTRATION (BVR) FUATIIA HAPA TUKIO ZIMA.

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Jaji mstaafu Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa hotel ya Vigimark mkoani Shinyanga,juu ya maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR). Alisema mfumo huo wa BVR utatumika wakati wa kuandikisha kwenye daftari na siyo kuhesabu kura na kuwataka watanzania kujitokeza kwenye vituo pindi zoezi litakapoanza kwani vitambulisho vya zamani havitatumika tena kwenye uchaguzi mkuu ujao. 
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mada iliyotolewa ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa BVR.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari,kutoka kulia ni Suleiman Abeid mwakilishi wa gazeti la majira Shinyanga, anayefuata ni Ester Mushi wa Tanzania daima akifuatiwa na Wezayi Ally kutoka Radio Faraja.

Afisa elimu ya mpiga kura kutoka NEC Salvatory Alute,akiwasilisha mada iliyotoa ufafanuzi wa maboresho ya daftari na kutumia mfumo wa Biometric Voter Registration (BVR) ,ambapo alisema taratibu zote zimeshakamilika huku akitaja idadi ya vituo vya kupigia kura kuongezeka kutoka 24,919 hadi 40,015 ambavyo vitatumika.  

mkutano bado unaendelea

Stephen Wang'anyi mwakilishi wa ITV mkoa wa Shinyanga ,akizungumza kwenye mkutano huo ambapo alitaka kupata ufafanuzi iwapo vitambulisho hivyo vipya vitamruhusu mtanzania kupiga kura kuchagua rais akiwa nje ya mkoa wake.

Mkutano bado unaendelea na waandishi wako makini kufuatilia ili kupata ufafanuzi zaidi.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Festo Kang'ombe akizungumza kwenye mkutano huo umuhimu wa mfumo wa BVR.

Waandishi wa habari wakiandika kwa umakini majibu ya ufafanuzi wa mfumo huo mpya wa teknolojia ya BVR ,mara baada ya mwenyekiti wa NEC kutoa ufafanuzi.

Mada iliyowasilishwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari na tume ya taifa ya uchaguzi NEC ,ikiwa ni maandalizi ya kuboresha daftari la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration(BVR).

No comments:

Post a Comment