Imeripotiwa
kuwa chui mwenye hasira na njaa aliingia majini na kupanda boti ya
mvuvi aliyetajwa kwa jina la Shushil Manjhi huko Kolkata, India na
kuondoka nae.
Taarifa
zilizoripotiwa na vituo vya nchini India vinaeleza kuwa, mvuvi huyo
alikuwa na watoto wake wawili (wa kike na wakiume) wakijaribu kutafuta
kitoweo karibu na hifadhi ya taifa ya Sunderbans yenye wanyama wakali.
Mwanae
wa kiume, Jyotish alieleza kwa njia ya simu kuwa chui huyo alirukia
boti na kumkamata baba yake shingoni kwa upande wa nyuma na kuanza
kumburuza akiondoka nae akielekea msituni.
“Alimrukia baba yangu kwa haraka mgogoni na kung’ata kwa nguvu kabla hajatokomea nae msituni.” Alieleza.
Mtoto
huyo anaeleza kuwa baada ya chui huyo kumkamata baba yake, yeye na
mdogo wake walijaribu kumpiga na fimbo na visu walivyokuwa navyo lakini
hakuweza kumuachia.
Tukio
hilo linatoa picha ya maisha duni ya wananchi masikini wa eneo hilo
ambao licha ya kuwa na hatari kubwa ya kuuawa na wanyama wakali, hali
ngumu ya maisha huwasukuma kuingia msituni kusaka kitoweo au chochote
licha ya kwamba ni kinyume cha sheria kufanya uvuvi katika eneo la
hifadhi ya wanyama.
Inaelezwa
kuwa samaki wanaopatikana katika hifadhi hiyo hunuliwa kwa pesa nyingi
katika miji ya jirani na vijiviji vya eneo hilo.
|
Saturday, June 28, 2014
CHUI ARUKIA BOTI NA KUTAFUNA MVUVI WANAE WASHINDWA KUMUOKOA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment