|
Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Warembo 20 wanaoshiriki shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga(Miss Shinyanga 2014) wakiongozwa na mwandaaji wa Mashindano hayo bi Asela Magaka wa Asela Promotions wametembelea kituo na kutoa msaada wa vyakula huku wakichangia kidogo walichokuwa nacho kwenye mifuko yao kuchangia ujenzi wa bweni katika kituo hicho chenye watoto zaidi ya 260.Pichani ni baadhi ya warembo wakiwa na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wakionesha upendo.
Misaada iliyotolewa na Asela Promotions na kukabidhiwa kwa mkuu wa kitengo cha Walemavu katika kituo cha Buhangija Jumuishi mwalimu Bright Mduma ni pamoja na,chumvi katoni 1, mchele kilo 100,unga wa sembe kilo 200,sukari kilo 20,mafuta ya kupikia lita 10,unga wa ngano kilo 50 na sabuni za unga za kufulia kilo 30, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 506,700/=
Watoto wenye ulemavu wakiwa katika eneo la tukio leo.
Aliyesimama ni mwandaaji wa Mashindano ya Miss Shinyanga mwaka 2014 bi Asela Magaka kutoka Asela Promotions,ambaye amekuwa akifanya maandalizi ya Mamiss Tangu mwaka 1999 akizungumza leo katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija mjini Shinyanga.Magaka alisema ameamua kuwapeleka warembo hao katika kituo hicho ili kujua mambo yanaoendelea katika jamii ikizingatiwa kuwa kauli mbiu ni “Urembo, sanaa na jamii” hivyo ni vyema wakajua kuwa urembo unahusiano na mambo ya jamii,wajue jamii inahitaji nini,na umuhimu wa kusaidia jamii,hii itasaidia warembo hawa kuwa mabalozi wazuri katika kusaidia watu mbalimbali wenye mahitaji maalum katika jamii.
Aliyesimama ni bwana Mustapha Ramadhani ambaye ni mwalimu wa Mamiss kanda ya ziwa akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo kufuatia changamoto ya mabweni aliahidi kuchangia mfuko 1 wa saruji kwa kuungana na Warembo 20 wanaoshiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2014 kuchangia mifuko 18 ya saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa bweni la wavulana lililoanza kujengwa 2013 na Miss Tanzania mwaka 2012 Brigette Alfred.
Kushoto ni mwandaaji wa shindano la Miss Shinyanga 2014 bi Asela Magaka kutoka Asela Promotions akikabidhi vyakula(moja ya mifuko ya unga wa sembe) kwa mkuu wa kitengo cha Walemavu katika kituo cha Buhangija Jumuishi mwalimu Bright Mduma
Baadhi ya washiriki Miss Shinyanga 2014-Kushoto ni bi Nyangi Warioba kutoka Msalala kulia ni bi Mary Emmanuel kutoka Ushetu ambao waliguswa na maisha ya watoto wenye ulemavu na kusababisha watokwe na machozi na kuamua kuchangia mifuko miwili ya saruji kuchangia ujenzi wa bweni lililoanza kujengwa na Miss Tanzani mwaka 2012 Brigette Alfred.Warembo wote 20 wameahidi kuchangia mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi huo ikiwa ni kukamilisha mifuko 18 ya saruji.
No comments:
Post a Comment