Wakinamama wajawazito na waliojifungua wakiwa katika wodi moja kwenye kituo cha afya cha Kambarage manispaa ya Shinyanga kutokana na upungufu wa wodi,hali ambayo inaweza kuhatarisha afya zao kwa kuambukizana magonjwa. Daktari
anayesimamia kituo hicho Costantine Hubby alisema
hali hiyo imesababisha wanaweke wajawazito na waliojifungua kulala wawili wawili kitanda
kimoja na wengine kulazimika kuweka magodoro sakafuni huku akitaja changamoto nyingine ni kituo kukosa chumba cha upasuaji wa dharura kwa
wajawazito wenye uchungu pingamizi
pamoja na kutokuwa na gari la wagonjwa hivyo kusababisha usumbufu mkubwa
mgonjwa akiwa amezidiwa hasa wakati wa msimu wa masika mvua zinaponyesha na
kuwa katika hatari iwapo atachelewa
kufikishwa kwenye huduma.
|
No comments:
Post a Comment