Tuesday, July 22, 2014

MWANAMKE AUWA MWANAYE KWA KUMNYONGA SHINGO NA KUMTUPA KWENYE KISIMA CHA MAJI HUKO KAHAMA


Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani humo.                                                                                                                                          

  story kamili.
 MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Rhoda Idetemya miaka 18 mkazi wa mtaa wa Nyasubi wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga amemuuwa mtoto wake mchanga mwenye umri wa miezi miwili kwa kumnyonga shingo  kisha mwili wake kutumbukiza kwenye kisima cha maji ya kunywa.
Mtoto aliyeuawa kinyama amejulikana kwa jina la Elizabeth Idetemya,ambapo tukio hilo lilitokea jana majira ya saa moja usiku katika mtaa wa Nyasubi Kahama.   
                                                  Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kuwa ,mwili wa mtoto huyo uligundulika wakati Ada  Patrick (25)alipokuwa  akichota maji kwenye kisima hicho kinachomolikiwa na Dkt.

Bakwili Salum ambaye anafanya kazi hospitali ya wilaya ya Kahama.                                                

Mtuhumiwa wa mauaji hayo ya kinyama alikamatwa na jeshi la polisi akiwa ndani ya gari wakati akijaribu kutoroka kwenda wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita ili kukwepa mkono wa sheria.
      Na Stella Ibengwe.

No comments:

Post a Comment