Mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Katika
hali ya kushangaza madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH), jijini Dar es Salaam walipigwa na butwaa baada ya mtoto Almasi
mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi kufikishwa hospitalini hapo
akiwa amekatwa seheme zake za siri na mtu aliyedaiwa ni mganga wa
kienyeji na kukimbilia kusikojulikana.
Akizungumza
kwa masikitiko makubwa wiki iliyopita, baba wa mtoto huyo, Ismail
Kamaga alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Kijiji cha
Omukagando, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Alisema mganga huyo aliyemtaja kwa jina moja la Adinali alifanya kitendo hicho kwa watoto wawili akidai anawafanyia tohara.
“Alidai
anawafanyia tohara watoto wawili, baada ya muda mwenzake alipona wa
kwangu hakuna kitu na nyeti aliondoka nayo, sina namna tena ya kumsaidia
mwanangu.
Nilimpeleka Hospitali ya Mugawa, Kagera ambako aliwekewa mpira wa kutolea haja ndogo na madaktari wakasema hawana jinsi.
“Pia nilikwenda Kituo cha Polisi Karagwe kuomba msaada wa kumkamata mtuhumiwa lakini imeshindikana,” alisema baba huyo
Mzazi
huyo aliiomba serikali kumtafuta mtuhumiwa akisema tukio alilolifanya
ni sawa na kuuondoa uhai wa mtu.Kwa upande wake, muuguzi wa zamu
aliyekuwa hospitalini hapo, Kulwa Kaombwe alisema kitendo kilichofanywa
na mtu huyo si cha kuvumiliwa akaiomba serikali kuchukuwa hatua ili
mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
“Kwa
ujumla huyu mtoto amebadilishiwa staili ya maisha na hicho ni kilema.
Kumkata uume maana yake mtoto huyo hatapata mke wala watoto katika
maisha yake,” alisema muuguzi huyo.
Kuhusu matibabu, alisema wanaendelea naye lakini tabu anayoipata Almasi ni kujisaidia kwa shida hasa haja kubwa.
No comments:
Post a Comment