Sherkhe wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu mara baada ya kumaliza kuswali swala ya Idd el- fitri,ambapo aliwataka kuendelea kuiombea nchi ili amani iliyopo iendelee kuwepo sanjari na mchakato wa kupata katiba mpya umalizike kwa amani na kuwepo maelewano kwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba.
Alisema wakati sasa umefika kwa
waumini wa dini hiyo na watanzania wote kuwaombea wajumbe wa bunge
maalumu la katiba ili waipitishe kwa amani na utulivu ,kwani
kumekuwepo na manung’uniko ya kutotendewa haki kwenye katiba ya sasa na kwamba katiba itakayo kuja
itapambanua haki za kila kiumbe.
“ Katiba hii haitapatika nje ya utaratibu uliopangwa ila kwa kupitia
sheria na kanuni zilizowekwa,
rai yangu kwenu ninawaasa kutokubaliana na nyumba za ibada zinazoanzisha
vurugu na kauli zenye misigano isiyo na tija katika taifa letu na kauli
zile zisizo watii viongozi wa kitaifa waliochaguliwa kwa kutumikia taifa hili”alisema
Sherkhe Makusanya.
Waislamu wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage
|
No comments:
Post a Comment