Wadau wa kiimo cha zao la pamba kutoka katika wilaya ya Itilima na Bariadi wakiwa kwenye mdahalo wa kujadili changamoto mbalimbali zinazolikabili zao la pamba mkoa wa Simiyu,ambapo wamezitaka mamlaka zinazohusika na zao hilo kuacha kukaa tu ofisini baadala yake waanze kuwatembelea wakulima vijijini ili kubaini changamoto zilizopo likiwemo suala la bei,mbegu na madawa ya kuuwa wadudu waharibifu. Wadau hao pia waliainisha changamoto mbalimbali ambazo zinachangia zao hilo kuendelea kutokuwa na ubora hivyo kukosa thamani kuwa ni pamoja na baadhi ya wakulima kuweka mchanga,sukari,chumvichumvi na maji ili kuongeza uzito kufidia kilo zinazoibwa kwenye mizani ya pamba. wakati wa kuuza kwa mawakala wa kampuni za kununua zao hilo.
|
No comments:
Post a Comment