Monday, July 14, 2014

WAZIRI WASIRA ATOBOA SIRI NZITO YA TANZANIA,BOFYA HAPA UPATE HABARI KAMILI

Waziri wa nchi,ofisi ya rais,mahusiano na uratibu Stephen Wasira akizungumza na waumini wa kanisa la romani katoliki Tinde mkoa wa Shinyanga ,wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa lililopewa jina la Papa John Paul wa II,Kwenye harambee hiyo Wasira alimuwakilisha waziri mkuu Mizengo Pinda ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi,ambapo aliwataka viongozi wa madhehebu ya dini kuendelea kushirikiana na serikali kuliombea taifa liendelee kuwa na amani kwani siri kubwa ya amani ni upendo,mshikamano na umoja wa watanzania.
Wanakwaya wakiimba wakati wa ibaada ya misa kabla ya kuanza harambee.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizungumza na waumini wa kanisa la romani katoliki pamoja na wageni waalikwa kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa.
Mapadrii wakiendelea na ibaada ya misa
Ibaada inaendelea
Waziri wa nchi,ofisi ya rais,mahusiano na uratibu Stephen Wasira akiweka jiwe la msingi kwenye jengo la kanisa ambalo linaendelea kujengwa,ambapo Wasira alimuwakilisha waziri mkuu Mizengo Pinda ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee hiyo.
Viongozi wakielekea eneo linapowekwa jiwe la msingi
Jiwe la msingi ambalo limewekwa na Waziri wa nchi,ofisi ya rais mahusiano na uratibu kwaniaba ya waziri mkuu Mizengo Pinda,ambaye alishindwa kufika kutokana na kuwa na majukumu mengine ya serikali.
Waziri Wasira akiwapongeza viongozi kwa kazi nzuri iliyofanyika.
Waziri wa nchi,ofisi ya rais,mahusiano na uratibu Stephen Wasira akizungumza na waumini wakati wa harambee iliyofanyika mji wa Tinde mkoani Shinyanga,ambapo alimuwakiisha waziri mkuu Mizengo Pinda.










No comments:

Post a Comment