Wednesday, July 16, 2014

MAMBO MAKUBWA YAIBUKA ZIARA YA UWT TAIFA MKOA WA SHINYANGA

Katibu mkuu wa umoja wa wanawake Tanzania UWT Amina Makilagi akizungumza na wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani humo kwa lengo la kutoa shukrani kwa wananchi kwa kuendelea kukipa ridhaa chama cha mapinduzi kutawala na kujionea kero zinazowakabili wananchi na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM ,ambapo alitumia fursa hiyo kuwaonya wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaoza watoto wao katika umri mdogo kwani huo ni ukatili wa kijinsia na kuwanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu. Pia alisema bado mikoa ya kanda ya ziwa inaendeleza vitendo vya ukatii kwa kuwauwa vikongwe wasiokua na hatia kutokana na imani za kishirikina  na kuwataka kuachana na imani hizo ambazo zinarudisha nyuma maendeleo.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Segese wilaya ya Kahama.
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya UWT taifa wakiwa katika ukumbi wa Bukwimba hoteli mji mdogo wa Maganzo wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga muda mfupi baada ya kupokelewa wakitokea mkoa jirani wa Simiyu.
Wanachama wa UWT wakiwakaribisha viongozi wao wa kitaifa katika mkoa wa Shinyanga ,huku wakionesha furaha waliyonayo.
Vija wa chipukizi wakiwa tayari kumpokea mgeni rasmi katibu mkuu wa UWT taifa mpakani mwa mkoa wa Shinyanga na Simiyu katika kijiji cha Wishiteleja wilaya ya Kishapu.
Mapokezi yanaendelea,ni wanachama na viongozi wa UWT mkoa wa Shinyanga wakimkaribisha katibu mkuu wa UWT taifa Amina Makilagi.
Kiongozi wa Uwt akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lyabukande wilaya ya Shinyanga

Hata ngoma zilikuwepo za kucheza na nyoka,hapa ni katika kata ya Didia wilaya ya Shinyanga.
Shughuli mbalimbali zilifanyika na hapa katibu mkuu UWT anawenka jiwe la msingi kwenye vibanda vya UWT wilaya ya Kahama ambavyo vinajengwa kwa ajili ya biashara kama kitenga uchumi cha umoja huo na kuacha kuwa tegemezi kwa kila jambo.   Katika kuunga mkono jitihada hizo aliahidi kugharamia vibada vitatu kuanzia msingi mpaka kukamilika ambapo kibanda kimoja kinagharimu sh 2.8 milion .mchango huo ni kutoa sapoti kwa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Azza Hamad ambaye tayari ameshachangia ujenzi wa vibanda vitatu. pamoja na gharama za vifaa vingine.
Zawadi pia zilikuwepo katika ziara hiyo wananchi walivutiwa na kuamuwa kutoa zawadi ya kuku kwa mgeni rasmi.
Wakinamama wakifurahia jambo
Diwani wa vitimaalum kata ya Didia wilaya ya Shinyanga akitoa neno la shukrani kwa viongozi wa UWT waliotembelea kata hiyo.
















No comments:

Post a Comment