Jeshi
la Polisi nchini Kikosi cha Usalama Barabarani limewafukuza kazi askari
27 baada ya kubainika kujihusisha na vitendo vya rushwa ikiwa ni sehemu
ya mkakati wa kuongeza nidhamu, uwajibikaji na maadili ya kazi kwa
askari polisi wa barabarani nchini.
Askari
hao wamefukuzwa kazi kuanzia Januari mwaka huu ambapo uamuzi huo ni
sehemu ya utekelezaji wa usimamizi wa nidhamu na mapambano dhidi ya
rushwa baada ya baadhi ya askari wa jeshi hilo kudaiwa kujihusisha zaidi
na vitendo hivyo.
Ni
katika mkutano na waandishi wa habari ndipo Kamanda wa Polisi Kikosi
cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga anasema usimamizi huo dhidi ya
vitendo vya rushwa umesaidia ongezeko la ukamataji wa makosa na
mabadiliko ya nidhamu za madereva kwenye matumizi ya barabara.
Akatoa
tathmini ya ajali za barabarani na kubainisha Mikoa iliyoongoza kwa
ajali nyingi kuanzia Januari mwaka huu ni Dar es Salaam yenye ajali
5,052 Morogoro ajali 514 huku Kilimanjaro ikiwa na ajali 332.
Hata
hivyo hali ya ukamataji wa makosa kwa madereva wasiopenda kutii sheria
bila shuruti yameongezeka kulinganisha na mwaka jana ambapo Januari hadi
Juni mwaka huu yamebainika makosa 515,677 huku Januari hadi Juni mwaka
jana yakiwa 301,404 ikiwa ni ongezeko la makosa 214,273 sawa na asilimia
71.
via>>fichuotz blog
No comments:
Post a Comment