Baadhi ya waendesha daladala za baiskeli manispaa ya Shinyanga wakiondoka eneo la mkutano .Picha kwa hisani ya Malunde blog. |
KUTOKANA na kukithiri vitendo vya ukatili kwa watoto wadogo kubakwa kisha kutoborewa
macho na baadhi ya waendesha daladala za baiskeli,baraza la madiwa la manispaa
ya Shinyanga limeazimia kuziondoa
daladala zote za baiskeli maeneo ya mjini ili kukabiliana tatizo hilo
pamoja na ajali huku zaidi ya matukio matano ya ukatili yameshatokea.
Baraza hilo lilifikia
uamuzi huo katika kikao chake kilichofanyika jana baada ya mchumi wa manispaa hiyo Christopher Nyarubamba, kutoa taarifa
ya kamati ya uchumi,afya na elimu
wakishauri kuondolewa daladala hizo kata za katikati ya mji na kutakiwa
kuwa kando ya mji kwa
kupatiwa usajili na kupewa vitambulisho pindi yanapotokea mtukio iwe rahisi kuwabaini.
Taarifa hiyo ya kamati alishauri kuondoa daladala na kutaja sababu
za msingi huku madiwani wakiunga mkono azimio hilo na kuwataka wananchi wa
manispaa kubadilika kama maeneo mengine kutumia daladala za magari kama ilivyo katika
maeneo mengine kwani niaibu mpaka sasa mji mzima unatumia daladala za baskeli wakati inaitwa
manispaa.
Wakichangia hoja hiyo baadhi ya madiwani Siri Yasin
(CHADEMA) na Shella Mshandete
(CCM) walisema hakuta wezekana
kuwafukuza waendesha daladala za baiskeli bila kufahamu mbadala
wake,hivyo inatakiwa usafiri upatikane ndipo zoezi la kuwaondoa lianze ,kwani
ndiyo tegemeo kubwa la usafiri waliouzoea
wananchi hivyo kuwakatisha ghafla
italeta tatizo.
“Hili jambo halipingiki
ni kweli kuna kero na kunamatukio mengi ya ukatili wa watoto yametokea kwa
kusababishwa na wandesha daladala,lakini mimi ninashauri tutafute kwanza
mbadala kabla ya kupiga marufuku daladala hizo,manispaa ikae na wamilii wa
magari kuona namna ambavyo wanaweza kutoa magari yakaanza kusafirisha watu
mitaa ya mjini”alisema Shella.
Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga
Boniface Chambi alisema kuwa daladala za gari zilikuwepo na
uzinduzi ulifanywa na mkuu wa mkoa Ally Rufunga , lakini cha kushangaza
watu walikuwa hawapandi hali iliyowakatisha tamaa wenye daladala hizo na
kuamua kusitisha mpaka sasa na kuendelea
kuonekana daladala za baiskeli pekee.
Awali Naibu mstahiki meya wa manispaa hiyo David
Nkulila alisema kuwa daladala za baiskeli ziondolewe kama
lilivyopitishwa azimio,huku akiwanyoshea kidole baadhi ya askari wenye
tabia ya kukamata magari ya abiria hovyo wakilenga mitazamo yao ya kimaslahi kuwa halitavumiliwa na kuwataka kuchukuwa hatua
pindi gari linapokuwa na tatizo.
No comments:
Post a Comment