Bi. Nasra Dafa (30) aliyeshambuliwa na mume wake wakati akiswali.
TUHUMA
nzito ya aina yake ambayo haijawahi kutokea ambapo mkazi mmoja wa
Tandale – Kwatumbo wilayani Kinondoni jijini, Idd Mpenda anadaiwa
kumshambulia na kumjeruhi hadi kuzimia mkewe, Nasra Dafa (30) wakati
akiswali.
Akizungumza
na Amani huku akimwaga machozi, mwanamke huyo alisema tukio hilo
lilijiri Julai 28, mwaka huu saa saba mchana wakati akiswali maeneo ya
duka lake lililopo Tandale.
ILIKUWA
KUSHTUKIZA ::Alidai kwamba alikuwa katika kusujudu, mara mumewe
alitokea na kumshambulia kwa mateke, ngumi na viatu kisha akamburuza
chini hadi nje hali iliyosababisha nguo aliyovaa kuvuka na kubaki kama
alivyozaliwa!“Kama unavyoniona, nimeumia sehemu mbalimbali za mwili.
Kiatu ndiyo kimeniumiza sana.
ATINGA KITUO CHA POLISI.
Alisema
baada ya tukio hilo kutokea alijivuta na kuvaa gauni lingine kisha
akakimbilia Kituo Kidogo cha Polisi Tandale ambapo polisi walimwambia
ishu yake ni nzito na kumtaka aende Kituo cha Polisi Magomeni (vyote
vipo Dar).
ASIMULIA VIPIGO, UKE WENZA.
Mwanamke
huyo aliweka hadharani kwamba mumewe amekuwa akimpiga mara kwa mara na
tatizo kubwa ni uke wenza ambapo alidai ameoa mke wa pili hivi karibuni
na mapenzi baina yao yamezorota.
“Mimi
kabla ya kufunga naye ndoa Januari Mosi, 2013 mume wangu alikuwa na mke
mwingine lakini aliamua kumpa talaka baada ya kumweleza kuwa mimi
sitaki kuwa mke mwenza. “Tukawa tunaishi naye lakini hata hivyo
hakuchukua muda mgogoro ukaanza ndani ya nyumba.
Picha hii ikionyesha majeraha ya mkononi na shingoni aliyopata Bi. Nasra Dafa.
SAKATA LAFIKA KWA NDUGU
Mwanamke
huyo aliendelea kusema kwamba hali ilizidi kuwa mbaya hadi ikafika kwa
wana ndugu kwa suluhu, walipatanishwa lakini baada ya muda mgogoro
ukaendelea na kuna siku mumewe akamwambia ameoa mke mwingine wiki tatu
nyuma.
SIKU YA TUKIO
“Siku
ya tukio, nilikuwa naswali. Unajua wakati wa Mfungo wa Ramadhani lazima
Muislam kuswali kwa kuzingatia taratibu zote za dini.
Basi,
alikuja na kuniita nitoke nje lakini sikutoka.“Niliona nimalize kwanza
kuswali ndipo nitoke, lakini kabla sijamaliza akaja na kunishambulia
kama niliovyokwambia kisha akachukua funguo na kufunga duka.
Amani
lilifika kwenye Kituo cha Polisi Magomeni na kuambiwa na askari mmoja
kuwa taarifa hizo zipo na mtuhumiwa anashikiliwa hapo, lakini akashauri
atafutwe Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura kwa
maelezo zaidi.
Kamanda huyo hakupatikana ofisini kwake hadi tunakwenda mtamboni.
SHEHE MKUU ASAKWA.
Shehe
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum hakupatikana
kuzungumzia makosa ya mume wa Kiislamu kumpiga mkewe wakati akiswali
ndani ya Mwezi Mtukufu.
Hata
hivyo, Maalim Hassan Yahya Hussein wa Magomeni Mwembechai alipoulizwa
alisema Uislamu haujatoa ruhusa kwa mwanaume kumpiga mkewe wakati
anaswali hata kama amefanya kosa kubwa kiasi gani.
“Uislamu
haujaruhusu kwa hali yoyote udhalilishaji na kuna hadithi zinazokataza
mtu kumdhuru mwenzake. Kuna masharti sita yamewekwa kabla ya mume
kufikia hatua ya kumwadabisha mkewe,” alisema Maalim Hassan.
Akaendelea:
“Kabla mume hajampa adhabu mke anapaswa kwanza kumpa nasaha kwa kosa
alilotenda na sharti la pili ni kumpa mawaidha ama yeye mwenyewe au
atafute mtu.
“Sharti
la tatu ni kumkumbusha mara kwa mara na sharti la nne ni kumhama
malazi, yaani kumuacha alale peke yake. Sharti la tano, akikosa ni
kwenda kushitaki kwa wazee au katika vyombo vya sheria ikiwemo kwa kadhi
na viongozi wa dini.“Sita ndiyo kumpiga, lakini kipigo ambacho
hakitamdhuru kwani hutakiwi kumpiga ukiwa na hasira.”
No comments:
Post a Comment