Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia askari wake wawili kwa
tuhuma za kumjeruhi kwa kumpiga risasi mwendesha piki piki aliyejulikana
kwa jina la Salgo Ndunguru(22) mkazi wa Ruvuma mjini Songea
Akizungumza kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela
amesema tukio hilo limetokea Agosti 26 mwaka huu majira ya saa 12 jioni
katika mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea ambapo askari polisi wawili PC
Waziri mwenye namba G 5075 na PC Ayoub mwenye namba G 9800 wakiwa doria
na piki piki ya polisi yenye namba za usajili PT 1250 CR aina ya Yamaha
CC 250 katika eneo hilo la Kombezi walimjeruhi mwendesha piki piki huyo
kwa kumpiga risasi.
Amesema mwendesha piki piki huyo alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na
askari PC Waziri katika harakati za kuinsuru silaha hiyo iliyokuwa
imebebwa na askari mwenzake PC Ayoub ambaye alizingirwa na baadhi ya
waendesha piki piki wakiongozwa na mwendesha piki piki aliyejulikana kwa
jina moja la Agrey ambaye alidai kuwa yeye ndiye mmiliki wapiki piki
iliyokamatwa na askari hao ikiwa imebeba mzigo wa majiko.
Ameitaja piki piki iliyokuwa ikiendeshwa na majeruhi huyo kuwa ni
aina ya San Lug yenye namba za usajili T 757 CUD ambapo baada ya
mwendesha piki piki huyo kukamtwa alimpigia simu mdhamini wake Agrey
alipofika alisababisha mkusanyiko mkubwa wa waendesha piki piki maarufu
kama Yebo yebo ambao walianza kuwarushia mawe askari hao huku majeruhi
akiwa ameshika mtutu wa bunduki iliyokuwa imebebwa na askari PC Ayoub
ndipo askari PC Waziri katika kuinusuru silaha isiporwe alimpiga risasi
majeruhi kwenye kiganja cha mkono wa kushoto na risasi hiyo kumjeruhi
sehemu mbili ambazo ni kiganja cha mkono wa kushoto na paja la mguu wa
kushoto.
Amesema majeruhi amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Ruvuma iliyopo mjini Songea kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri
na katika vurugu hizo zilizodumu kwa muda wa nusu saa kabla ya kutulizwa
na kikundi cha askari maalumu kilichowahi na kutuliza vurugu hizo kwa
kutumia nguvu kidogo hali ikarejea kuwa shwari nahakuna madhara zaidi
yaliyojitokeza.
Aidha kamanda Msikhela amesema uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio
hilo unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo unaendelea na
hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika watakaothibitika na ametoa wito
kwa waendesha piki piki kuacha tabia ya kushabikia vurugu ambazo hazina
tija na kuwa chanzo cha kusababisha migogoro isiyokuwa na maana na
kusababisha madhara kwa jamii.
Amewataka waendesha piki piki kufuata taratibu zilizopo ikiwa ni
pamoja na kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi husika kwa kupitia
viongozi wao ili yaweze kufanyiwa kazi amewataka wananchi mkoani Ruvuma
kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao bila hofu yoyote kwani jeshi
la polisi liko imara kulinda mali na maisha yao.
story :Na Nathan Mtega wa demashonews,Songeay .
No comments:
Post a Comment