|
Aliyevaa
suti ya kijivu ndiyo askofu wa kanda Rafael Machimu aliyefikishwa
mahakamani kwa kosa la kufukuza wachungaji kinyume na katiba ya kanisa
kwa maslahi yake binafsi,na hapo katika picha akiwa na wapambe wake
akitoka mahakamani .
|
|
Waumini
wa kanisa la EAGT Majengo manispaa ya Shinyanga wakimshangilia
mchungaji wao David Mabushi baada ya kushinda kesi ndogo kupinga
kuvuliwa uongozi wake ndani ya kanisa hilo.Kesi hiyo ilifunguliwa na
waumini wa kanisa hilo wakishirikiana na mchungaji huyo dhidi ya
kumpinga askofu wa kanda ya magharibi Rafael Machimu ambaye
aliwafukuza wachungaji wanane na kulaumiwa na waumini ambapo kesi hiyo
iliendeshwa mahakama ya wilaya shinyanga chini ya hakimu Thomson Mtani
ikiwa kesi ndogo imekwisha na kesi ya msingi itaanza kusikilizwa tarehe
29/septemba mwaka huu na kesi ndogo imekwisha tolewa maamuzi kuwa
mchungaji huyo aendelee na kazi yake kama kawaida.
|
|
Waumini
wa kanisa la EAGT wakiwa wamembeba mchungaji wao David Mabushi baada
ya kuruhusiwa na mahakama kuendelea na uchungaji wa kondoo wa mungu
mpaka pale kesi yake ya msingi itakaposikilizwa tena,hapo pichani wakiwa
nje ya kanisa baada ya kutoka mahakamani.
|
|
Hapo waumini wakimpokea mchungaji wakati akitoka mahakamani na kuelekea kanisani. |
wakiendelea kuchangilia kwa kushinda kesi ndogo.
|
Waumini
wa kanisa la EAGT wakitoka nje ya mahakama ya wilaya ya Shinyanga huku
wakiwa na nyuso za furaha baada ya mchungaji wao kuruhusiwa kuendelea
na shughuli za uchungaji mpaka pale kesi ya msingi itakapo malizika. |
Umati wa waumini uliokuwa ukisubiria nje ya mahakama .
|
Huyu
Askofu Rafael Machimu aliyekuwa natuhumiwa na waumini wake kwa kuchukua maamuzi yake bila
kufutata katiba ya EAGT na kuwafukuza wachungaji ambapo ndio alikuwa
akienda mahakamani kwa furahama. |
|
waumini wasema ushindi katiba lazima ifuatwe. |
|
Askofu
Machimu akiwa na mke wake mwenye nguo za rangi ya njano na bluu pamoja
na wapambe wake akiwa nje ya mahakama ya wilaya siku ya jumatatu
wakisubiri shauri dogo nje ya mahakama ya wilaya ya Shinyanga mwanzoni
mwa wiki hii.-Picha zote na Chibura Makorongo-Shinyanga |
No comments:
Post a Comment