JESHI la Polisi Wilaya
ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, linamtafuta mkazi wa Malangali, Bw. Saimon
Paskali kwa kosa la kuwapiga watoto wake, kumuua mmoja na kukimbia
kusikojulikana.
Tukiio hilo limetokea
usiku wa kuamkia jana baada ya mtuhumiwa kurudi nyumbani akitokea kwenye
Sherehe ya Komonio akiwa amelewa na kuanza kuwapiga watoto wake kwa
fimbo hadi wakazirai.
Akizungumzia tukio
hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Frednandi Rwegasila, alisema
mtuhumiwa alikuwa akiishi na watoto muda mrefu baada ya kuachana na
mkewe.
Aliwataja watoto hao
kuwa ni Daniel Paskali (11) ambaye ndiye aliyefariki na Jackson Paskali
(9) ambao baada ya kuzirai kwa kipigo na mtuhumiwa kukimbia, majirani
walikwenda kutoa msaada wa kuwapeleka hospitali.
"Wakiwa njiani, Paskali
alifariki dunia wakati Jackson amelazwa katika Hospitali ya Mkoa
akiendelea kupatiwa matibabu na ameumizwa sehemu mbalimbali ya mwili
wake," alisema.
Kamanda Rwegasila alisema jeshi hilo linaendelea kumsaka mtuhumiwa ili aweze kufikishwa mahakamani.
Chanzo:Majira.
No comments:
Post a Comment