Wednesday, August 13, 2014

AFISA MTENDAJI ASIMAMISHWA KAZI KWA UZEMBE NA UBADHILIFU WA FEDHA ZA MRADI WA MAJI


Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Songambele kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakichota maji ukiwa ni mradi wa ziwa victoria ambao umesababisha watu wanne wajumbe wa kamati ya maji iliyokuwa ikisimamia mradi kufikishwa mahakamani kutokana na ubadhilifu wa sh milion nane ambazo zinatokana na mauzo ya maji.Hata hivyo afisa mtendaji wa kijiji hicho Paschal Chuma naye amesimamishwa kazi kutokana na uzembe pamoja na kushindwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi yatokanayo na mradi huo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008.


  Katika mradi huo wa maji inadaiwa na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kuwa  kwa mwezi walikuwa wakikusanya kiasi cha shilingi millioni 1.6 katika kituo kikubwa  na kituo kidogo ni kiasi cha shilingi millioni 1.5, lakini katika akaunti ya benki kulikuwa  na kiasi cha shilingi laki tatu  tangu mradi huo  ulipozinduliwa mwezi wa tano mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment