Thursday, August 14, 2014

YALIYOJIRI SHINYANGA HAYA HAPA PATATUKIO ZIMA NA PICHA


Kulia ni mratibu wa afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri ya mji Kahama Jerome Onesmo ambaye alisema  mwitikio wa akina mama kufika katika hospitali ya wilaya ya Kahama ni asilimia 100 kwani kila siku wamekuwa wakipokea akina mama zaidi ya 40 wanaofika kupima afya zao kwa hiari huku akipongeza kazi nzuri ya EGPAF na AGPAHI katika kusaidia jamii kwani wamekuwa wakitoa pia vifaa tiba kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi na uzazi wa mpango.


Hapa ni ndani ya ofisi ya kaimu mganga mkuu halmashauri ya mji Kahama mkoani Shinyanga Dkt John Fabian Ng'home(pichani).

Hapa anazungumza na waandishi wa habari walioambatana na mratibu wa kitengo cha mawasiliano na utetezi shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) Mercy Nyanda katika ziara yake ya siku 4 mkoani Shinyanga,kufanya tathamini kuhusu miradi inayosimamiwa na shirika hilo mkoani Shinyanga,ambapo anakutana na wataalam wa afya na wananchi walionufaika kupitia shirika hilo, AGPAF ni shirika linalojihusisha na kutokomeza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto likifadhiliwa na watu wa Marekani kupitia shirika la USAID na CDC.

Dkt Ng'home alisema hospitali ya wilaya ya Kahama ni miongoni mwa vituo vitatu(vingine ni hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kituo cha afya cha Nindo) mkoani Shinyanga vinavyosaidiwa na EGPAF na AGPAHI 
kuhusu huduma ya uzazi wa mpango,uchunguzi kuhusu saratani ya shingo ya kizazi na kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Kushoto ni mratibu wa kudhibiti UKIMWI katika halmashauri ya mji wa Kahama Dkt Ayamery Mlay akizungumzia kuhusu mkakati wa kutokomeza maambukizai kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ambapo alisema kila mjamzito akifika katika hospitali kwa mara ya kwanza hupimwa vvu na akibainika kuwa navyo basi huanzishiwa matibabu/chanjo mara moja ili kumkinga mtoto asiambukizwe.


Dkt Ayamery Mlay alitumia fursa hiyo pia kuwataka akina mama kuacha kujifungulia majumbani na kwa wakunga wa jadi huku akieleza changamoto kubwa inayowakabili sasa kuwa ni upatikanaji wa damu salama.




Wataalam wa afya ya uzazi wakizungumza na waandishi wa habari juu ya huduma ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi,uzazi wa mpango pamoja na mkakati wa kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.Waliliomba shirika la EGPAF na AGPAHI kuendelea kuwajengea uwezo wataalam wa afya na kutoa vifaa tiba kwani mji wa Kahama umekuwa na mwingiliano wa watu wengi na wengi wamekuwa wakifika katika hospitali hiyo na kujikuta ikizidiwa kwa kuwa na wateja wengi


Kushoto ni mratibu wa afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri ya mji Kahama Jerome Onesmo akisistiza kuhusu umuhim wa wanaume kwenda na wake zao/wenza wao katika hospitali na vituo vya afya(Kahama viko 17),ingawa aliiomba serikali na wadau kuongeza idadi ya vituo vya afya katika wilaya hiyo.Kulia kwake ni mratibu wa kitengo cha mawasiliano na utetezi shirika la EGPAF Mercy Nyanda


Wataalam wa afya wakiwemo wauguzi na wakunga  ambao walisema wamekuwa wakipokea wateja wengi ukilinganisha na idadi ya watumishi waliopo

Kushoto ni mratibu wa kitengo cha mawasiliano na utetezi shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) Mercy Nyanda akiwa na waandishi wa habari Herman Meza(The Guardian) na Grayson Kakuru(TBC) ndani ya jengo la kitengo cha afya uzazi

Ziara katika Kituo cha afya cha Nindo wilaya ya Shinyanga_Kituo cha afya cha Nindo ni miongoni mwa vituo vinavyotoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi,mbali na hospitali ya mkoa wa Shinyanga na hospitali ya wilaya ya Kahama vikisimamiwa na AGPAF na AGPAHI wakishirikiana na serikali.Lakini hapa Nindo huduma za uzazi wa mpango na kuzuia maambukizi ya vvu kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto zinapatikana katika kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na afya njema

Mwandishi wa habari Anceth Nyahore gazeti la Nipashe (katikati) akizungumza na akina mama katika kituo cha afya cha Nindo waliofika hapo kwa huduma mbalimbali za afya ikiwemo uzazi wa mpango


Kushoto ni mwandishi wa habari Shaaban Alley Star tv akifanya mahojiano na bi Rosemary ambaye alisema wanaume wengi wana uelewa mdogo kuhusu uzazi wa mpango hali ambayo inachangia kuongezeka kwa watoto katika jamii.Hata hivyo alisema wanawake wengi sasa wameelimika na wameanza kutumia uzazi wa mpango japokuwa kwa siri ili waume zao wasijue na kujikuta wakiachika kwani wanaume wengi wanapenda wake zao wazae kila mwaka


Waandishi wa habari pamoja na mratibu wa kitengo cha mawasiliano na utetezi shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) Mercy Nyanda (kulia) wakizungumza na wakazi wa kijiji cha Busombo/Iselamagazi  wilaya ya Shinyanga kuhusu masuala ya uzazi wa mpango na changamoto wanazokabiliana nazo


No comments:

Post a Comment