Friday, August 15, 2014

DENI LA SH MILION 140 LA IPONZA TFF BASI LAKE LAMATWA KWA AMRI YA MAHAKAMA.

Basi la wachezaji wa soka TZ lakamatwa ili kulipa madeni
Basi la wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, limekamatwa kwa amri ya mahakama kutokana na deni la shilingi milioni 140 (zaidi ya dola 85,000), ambalo kampuni ya Punchline kutoka Kenya, inadaiwa kulidai shirikisho la kabumbu Tanzania (TFF).
Madalali ndiyo walilikamata basi hilo likiwa kama dhamana huku TFF ikitakiwa kulipa deni husika kabla ya kurejeshewa mali zao.
Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, amesema tayari wamelipa shilingi millioni 70 ikiwa ni malipo ya awali.
Deni hilo linatokana na gharama za uchapishaji tiketi za kuingilia uwanjani katika mechi za ligi kuu ya Tanzania tangu mwaka 1997.
TFF kwa sasa iko katika mpango wa kuuza tiketi za uwanjani kwa njia ya ki-eletroniki (umeme) ikiwa ni sehemu ya jitihada ya kupunguza adha kwa wapenzi wa soka na kudhibiti wizi na ulanguzi wa tiketi.
Wambura amesema jitihada zinafanyika kumaliza deni hilo, ila TFF italifuatilia kwa umakini na kuchunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.

No comments:

Post a Comment