Friday, July 25, 2014

MFANYAKAZI WA NDANI AUAWA KWA KUNYONGWA KWA KANGA

MFANYAKAZI wa ndani aliyefahamika kwa jina la Eliwaza Damiano mwenye umri wa miaka 15 mkazi wa mtaa wa Majengo mapya manispaa ya Shinyanga ,amekutwa amekufa ndani ya chumba chake baada ya kunyongwa na watu wasiojulikana kwa kutumia kipande cha kanga.                                                      Taarifa iliyotolewa leo na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha imesema kuwa mfanyakazi huyo alikutwa na mwajiri wake akiwa amekufa jana majira ya saa moja jioni ,huku uchunguzi wa awali ukionyesha kuwa marehemu alinyongwa kwa kutumia kanga na watu wasiojulikana ambao baada ya kufanya mauaji waliiba Laptop moja na mkoba wa mkononi uliokuwa na kiasi cha sh 20,000/=.                                               Kamanda Kamugisha alisema marehemu alikuwa akifanya kazi za ndani kwa Elizabeth Joseph miaka 38 mfanyakazi wa benki ya CRDB na kwamba wanaendelea na upelelezi ili kuwapata waliohusika na tukio hilo huku akitoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kuwabaini na kuwakamata wahusika mauaji .
 Stellahomolwa.blogspot.com

No comments:

Post a Comment