Friday, July 25, 2014

MAJERUHI SITA WA AJALI YA FUSO WAMEPELEKWA HOSPITALI YA BUGANDO ,MWANZA KWA MATIBABU ZAIDI MAJINA YAO HAYA HAPA.

Wananchi wakiangalia fuso  ambalo jana liliacha njia na kupinduka katika kijiji cha Uchunga wilaya ya kishapu mkoani Shinyanga na kuuwa watu watatu huku 46 wakiwa ni majeruhi wakati likielekea kwenye mnada wa Mhunze ambapo wengi waliokuwa ndani ya gari hilo ni wafanyabiashara.                                                                                                                            Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi ,Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Maguja Daniel alitaja  majina ya waliopelekwa na umri wao na kwenye mabano ni sehemu wanayotoka kuwa ni  Masanja Kishiwa 42(Mwajiginya)Mayala Lugomela 31(Jijongo)Malando Mashamindi20(Nobola) Marco Bundala 19(Jijongo) Geremia Jisena 35(Mwaweja) na Ndila Shigela 41 kutoka kijiji cha Mwajiginya wote ni wilaya ya Kishapu.                                                   Waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni watatu ambao ni Charles Makengwa,  Difa Shimo miaka 28 wote wakazi wa wilaya ya Kishapu ambapo maiti moja ndugu zake bado hawajapatikana ili kuitambua.                                                          Na Stellahomolwa.blogspot.com

No comments:

Post a Comment