Friday, July 25, 2014

PATA TUKIO ZIMA NA PICHA ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA MKOA WA SHINYANGA

Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annarose Nyamubi akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo katika maadhimisho ya siku ya mashujaa ambayo yamefanyika mazingira centre  eneo ulipojengwa mnara wa kumbukumbu ya mashujaa .
Mhasibu mkuu wa serikali mkoa wa Shinyanga Burton Mwakanyamale akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa mji
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamu Hafidhi akiweka upinde na mkuki ikiwa ni kuashiria kuwakumbuka mashujaa waliopigana vita ya pili ya dunia
Afisa uhamiaji mkoa wa Shinyanga Annamaria Yondani akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa.
 Mzee Omari Mbushi mkazi wa kijiji cha Bugayambelele manispaa ya Shinyanga, ambaye alipigana vita ya pili ya dunia akiweka shoka kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
Viongozi wa madhehebu ya dini na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
Wananchi na viongozi wa mkoa wa wakiwa kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa ambao ulijengwa mwaka 1972 mazingira centre manispaa ya Shinyanga.
Maadhimisho yanaendelea
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annarose Nyamubi ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo,akiweka ngao kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa katika viwanja vya mazingira centre mjini Shinyanga.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga
Viongozi wa serikali wakiwa eneo ulipojengwa mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.










+

No comments:

Post a Comment