Thursday, July 24, 2014

IDADI YA WALIOKUFA AJALI YA FUSO KISHAPU WAFIKIA WATATU NA MAJERUHI 46

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga  Justus Kamugisha akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ambapo amesema katika ajali iliyotokea leo asubuhi kijiji cha Uchunga wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga, idadi ya majeruhi imefikia 46 huku waliopoteza maisha wakiwa ni watu watatu.                                                Kamugisha alisema gari hilo aina ya fuso lenye namba za usajili T680 ARL
mali ya Ngasa Seni mkazi wa kijiji cha Kiloleli wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga  .
  lilikuwalikitoka kijiji cha Kiloleli wilayani humo kuelekea kwenye mnada wa Mhunze lilipofika kijiji cha Uchunga kilomita chache kufika Mhenze lilipinduka huku dereva wake akikimbia baada ya ajali kutokea.             , Alisema majeruhi  35 wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na wengine  11 wako hospitali ya Kolandoto  katika manispaa hiyo na kwamba gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Shija Ngassa mkazi wa kijiji cha Kiloleli Kishapu.                                Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel amesema wamepokea miili miwili ya marehemu na mwingine mmoja alifariki wakati akipatiwa matibabu na majeruhi 35 na wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.                  

No comments:

Post a Comment