Sunday, August 24, 2014

YALIYOJIRI MKUTANO WA CHAMA CHA ACT-TANZANIA SHINYANGA HAYA HAPA

Wananchi wa manispaa ya Shinyanga wakichukua kadi za chama kipya cha siasa cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara ambao ni wa kwanza katika mikoa ya kanda ya ziwa uliofanyika viwanja vya mahakama ya mwanzo mkoani Shinyanga .
Wananchi wakichukuwa kadi za chama cha ACT-Tanzania alizokuwa anazitoa mwenyekiti wa chama hicho taifa Kadawi Limbu.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.
 Mwenyekiti wa taifa wa chama cha ACT -Tanzania Kadawi Limbu akizungumza na wananchi wa manspaa ya Shinyanga ,alisema chama hicho kitakuwa ni mkombozi mkubwa wa watanzania katika kukabiliana na changamoto zilizopo likiwemo suala la rushwa kwa kuchukua hatua kwa watu watakao husika .ambapo pia alitumia fursa hiyo kuweka wazi kuwa ACT haina ubia na CCM wala mpango wowote wa kushirikiana nao
Mjumbe wa halmashauri kuu taifa ACT-Tanzania Athuman Balozi kutoka mkoa wa Tabora akizungumza na wakazi wa manispaa ya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara.
Viongozi wa ACT-Tanzania wakiwa meza kuu mara baada ya mwenyekiti wa chama hicho taifa kuwasili uwanjani.
Katibu wa vijana  taifa  ACT-Tanzania Philip Malaki akiwaasa wakazi wa manispaa ya Shinyanga kutoa ushirikiano na kukiunga mkono chama hicho katika kuleta mabadiliko kwa watanzania huku akiwataka kuwa makini na wanasiasa kwani wanawatumia kama sehemu ya kufanikisha masuala yao na kupata madaraka.
Msafara wa mwenyekiti wa ACT-Tanzania ukiwasili eneo la mkutano ukiwa umetanguliwa na piki piki.
Gari la chama cha ACT -Tanzania
Mratibu wa ACT-Tanzania mkoa wa Shinyanga Benedict Kishija akizungumza na wakazi wa manispaa ya Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wanaendelea kutoa salamu za ACT-Tanzania kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga,jukwaani ni Idd Mapande kutoka wilaya ya Kahama.
Mkutano unaendelea
Wananchi
Mwenyekiti wa ACT- Tanzania mkoa wa Shinyanga Justina Kimisha akieleza sera za chama hicho.(Picha zote na Stella blog)
                                      
                                             













No comments:

Post a Comment