Monday, August 25, 2014

VIONGOZI WAPYA WACHADEMA MKOA WA SHINYANGA HAWA HAPA.

Mbunge wa Maswa mashariki kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa Simiyu Syliveter Kasulumbayi (Picha na Maktaba ya Stella Blog).
     
Takribani miaka mitatu imepita Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),mkoani Shinyanga kilikuwa hakina mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho baada ya aliyekuwa mwenyekiti kufariki  dunia marehemu Philip Shelembi,hatimaye  kimepata viongozi wapya.

  Uchaguzi huo ulisimamiwa na Kasulumbayi uliofanyika mjini Shinyanga, alisema lengo la uchaguzi ni kuendelea kuimarisha chama  na kujipanga katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015.

Kasulumbayi aliwataja viongozi hao wapya waliochaguliwa kuwa ni Peter Frank,Mwenyekiti wa Chadema mkoa, katibu ni Zacharia Thomas, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), Chripin Simon, Katibu BAVICHA ni Ezekiel Joseph.

Kwa upande wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA),mwenyekiti ni Rachel Mashishanga,  Mbunge wa viti maalum (CHADEMA),jimbo la Shinyanga Mjini na katibu wake Winfrida Daudi huku mwenyekiti wa baraza la wazee mkoa akichaguliwa Mhidini Ibrahim.

No comments:

Post a Comment