Hii ndiyo habari kamili.
MADIWANI wawili wa chama cha Demokrasi na maendeleo
(CHADEMA)waliojiuzuru nyadhifa zao mapema mwaka huu kisha kujiunga na CCM,
hatimaye wamerudi tena Chadema huku wakitoboa siri iliyofanya waondoke kuwa
waliahidiwa watapelekwa chama kipya cha Alliance for Change and Transparency (ACT-
Tanzani na kudai kuwa mpango huo ulihusisha vigogo wengine wa chama hicho.
Wakizungumza jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja
vya mahakama ya mwanzo manispaa ya Shinyanga ulioandaliwa na CHADEMA,madiwani
hao waliojiuzuru Sebastian Peter kata ya Ngokolo na Zacharia Mfuko kata
ya Masekelo walisema wao walikuwa ni watu wa kwanza kuondoka lakini mikakati
hiyo waliipanga na viongozi wengine kubwa ndani ya chama ili wakajiunge na
chama kipya cha ACT waweze kukijenga.
Sebastian alisema baada kuondoka walijua wataingia moja kwa moja
ACT lakini hali ilikuwa tofauti kutokana na kutakiwa kujiunga kwanza CCM ndipo
wapate nafasi ya kwenda huko,jambo ambalo waligundua kuwa wamechezewa kamali
kisha kuamuwa kurudi kuwaomba msamaha wanachama na wananchi ili wawapoke
kwani walichobaini ni michezo ya kisiasa ya kutaka kuharibiana.
“Ninashangaa sana kuona hapa viongozi wengine wanatuponda wakati
wote tulikuwa kwenye mkakati huo wa kuondoka Chadema kwenda ACT, sisi
tulitangulia kwenda kuangalia mazingira kama ni mazuri ili na wao wafuate
lakini tulichokikuta huko mmbo siyo mazuri ninawasihi achaneni na mpango huo
huko hapafai bora Chadema na ndiyo maana tumerudi”alisma Peter.
Hata hivyo mara baada ya kufika eneo la mkutano madiwani hao
waliojiuzuru waliamsha hasira kwa wananchi na wanachama ambao waitaka
waondoke eneo hilo kwa kuwa ni wasaliti wakubwa wa Chadem, hivyo hawahitaji
kuwaona,ndipo mbunge wa chama hicho jimbo la Maswa mashariki Sylivester
Kasulumbayi ilimlazimu kuingilia kati kuwatuliza kisha mkutano kuendelea.
Madiwani hao walifika kwenye mkutano huo wakiwa wamebebwa kwenye
piki piki huku wamevaa sare za CCM baada ya wanachi kushusha hasira waliwapa
fursa ya kujieleza kila mmoja,kisha waliondolewa kwa gari kabla mkutano
haujaisha kwa ajili ya usalama wao ili kuepusha vurugu kutokea.
Naye Zacharia Mfuko mmoja wa waliojiuzuru alilihusisha tukio la
kuondoka kwake kuwa zilitumika nguvu za giza kuwachanganya akili na kuamuwa kuondoka
Chadema ,kwani mpaka sasa anajutia hatua aliyoichukuwa ya kwenda CCM na
kuwaomba wanachama wampokee kwa kuwa bado ana mambo mengi ya kueleza mchakato
ulivyokuwa ukifanyika wa kukibomoa chama hicho.
Alisema kuna baadhi ya viongozi wa CCM wakubwa walihusika katika
kuwarubuni ili wahamie huko na baada ya kufanikiwa kuwapata waliwachukuwa
wakawapeleka jijini Dar es salaam ambako walikutana na viongozi wengine kisha
kurudishwa Dodoma na kuendelea na mikakati ya kupata wanachama wengi zaidi
watakaokwenda kuijenga ACT.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Maswa mashariki Sylvester
Kasulumbayi aliwataka wananchama wa Chadema kuwapokea huku akisema walirubuniwa
na kwamba hatua hiyo itawawezesha kufahamu zaidi mambo yaiyokuwa yamejificha
ili waweze kuyafanyia kazi ili kukijenga chama na kuwa imara zaidi badala ya
kuwa na mpasuko.
“Ndugu zangu mhalifu akikamatwa huwa hawamuuwi unamuacha ili akupe
taarifa zaidi za wahalifu wengine kwa hiyo na mimi ninawaomba sana
wanachadema wenzangu tuwapokee walifanya hivyo kimakosa,tusiwe na
hasira ili tuweze kufahamu mambo mengi zaidi yaliyokuwa
yamejificha”alisema Kasulumbayi.
Na Stella blog.
No comments:
Post a Comment