Saturday, August 30, 2014

JWTZ WAFANYA USAFI NA KUTOA MSAADA KITUO CHA WALEMAVU BUHANGIJA SHINYANGA


Mlezi wa kituo cha Buhangija kinacholelea watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga Zainab Husein ,akimshukuru mkuu wa kikosi cha jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ), kikosi cha 516  kambi ya kizumbi iliyopo manispaa ya Shinyanga Luteni Kanali Mussa Kingai baada ya kutoa msaada wa chakula na kufanya usafi kwenye kituo hicho wakiwa wanaelekea kuadhimisha miaka hamsini ya kuundwa kwa jeshi hilo hapa nchini(1964).
Viongozi wa kituo cha Buhangija wakiwa na mkuu wa kikosi cha 516 kambi ya kizumbi.
Mkuu wa kikosi cha 516 kambi ya Kizumbi iliyopo manispaa ya Shinyanga Luteni Kanali Mussa Kingai,akizungumza na watoto pamoja na viongozi wa kambi hiyo ,ambapo aliahidi kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto wenye ulemavu  wa ngozi Albino sanjari na kuitaka jamii kushirikiana na kukemea vitendo hivyo.
Wanajeshi wakifanya usafi wa mazingira katika kituo cha Buhangija kinacholea watoto wasioona,walemavu wa viungo,wasiosikia na Albino.
Sehemu ya misaada iliyotolewa na kikosi cha 516 kambi ya Kizumbi.
Watoto wenye ulemavu wa ngozi Albino wakiwa katika eneo la kituo chao wanapolelewa.
Misaada iliyotolewa na kikosi hicho ni pamoja na kilo 50 za sukari,mafuta ya kupaka cartoni mbili,ndoo mbili za mafuta ya kupikia,kilo 25 za unga wa sembe ,majani ya chai,chumvi,sabuni za kufulia pamoja na mbuzi wawili.

Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wakiwa na wanajeshi kikosi cha 516 kambi ya Kizumbi.

                                     







No comments:

Post a Comment