Tuesday, August 5, 2014

MASIKINI WANAFUNZI HAWA NA WALIMU WAO ONA WANAVYOTESEKA SERIKALI ICHUKUWE HATUA.

WANAFUNZI wanaosoma katika shule ya msingi  Mawemilu iliyopo  kata ya Mwakitolyo  halmashauri ya wilaya ya  Shinyanga wanajisaidia vichakani kutokana na ukosefu wa vyoo vya kutosha , huku
walimu wakilazimika kwenda kutumia vyoo vya familia ya walimu ambazo ziko jirani na shule hiyo hali ambayo inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa.
Moja ya darasa lililopo katika shule ya msingi Mawemilu kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,likiwa halina hata dawati mmoja wanafunzi wake wanakalia magogo ya miti na mawe.
Hali hiyo ilibainika jana baada ya waandishi wa habari kutembelea shule hiyo  yenye jumla ya wanafunzi 511 na walimu 11 na kujionea hali halisi ,huku vinyesi vikiwa vimetapakaa nje vya vyoo viwili vilivyoezwa kwa nyasi  ambavyo vinatumika kwa sasa pia havikidhi mahitajikutokana na idadi ya wanafunzi.
 
 Mwalimu mkuu wa shule hiyo  Joseph Chagaka akizungumza na waandishi wa habari alikiri kuwepo kwa  changamoto hizo  huku akisema   awali kulikuwepo na  matundu ya vyoo sita kwa wanafunzi, lakini yalititia  kutokana na mvua za masika zilizokuwa zikinyesha na kwamba  upande wa vyoo vya walimu  hakuna hivyo kufanya kazi katika mazingira magumu.
 “Tunachangamoto kubwa katika shule hii, tuliamua kujenga choo hicho chenye matundu mawili kwa kutumia nyasi  ili   wanafunzi watumie kwa  muda tukiwa tunaendelea kujipanga na ujenzi mwingine wa kudumu,nina amini havitoshelezi kukidhi mahitaji  kwani kuna wanafunzi 511 ,kwa ujumla hali siyo nzuri tunahitaji serikali itusaidie’’alisema Chagaka.
Hiki ni choo cha wanafunzi ambacho kimeezekwa kwa nyasi kinamatundu mawili na kinatumiwa na wanafunzi zaidi ya 500 wa shule hiyo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo alisema madawati  yaliyopo ni  50 ambayo hayatoshi hivyo kusababisha robo tatu ya wanafunzi kukaa kwenye magogo na wengine kutumia  mawe.
 
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji hicho  Ezekiel  Deusi alisema  changamoto kubwa shuleni hapo ni vyoo  kwani  miundombinu yake ni mibovu ni sawa na hakuna vyoo , vilivyokuwepo vilititia kipindi cha mvua  za masika na sasa wanahitaji matundu  11 ili kuondoa changamoto hiyo .
 
Hata hivyo  afisa elimu msingi Andrew  Mitumba  wa halmashauri hiyo  alisema kuwa kero hiyo ni  ya muda mrefu kwani mwalimu mkuu wa shule hiyo  alikwisha andikiwa barua ya  onyo kutokana na  uzembe.
“Huu ni uzembe wa viongozi na  serikali ya kijiji, isitoshe  kuna  fedha za ruzuku hutolewa kwa shule za msingi ambazo anatakiwa  achukue kidogo na kuanzisha ujenzi na kuchangisha  michango kwa wananchi , ili halmashauri iweze kukamilisha kwa kuezeka maboma lakini  huyu mwalimu mkuu hafanyi hivyo kama alivyoelekezwa,pia suala la  ukosefu wa madawati tayari watapatiwa muda si mrefu
                                       Na Stella blog.

No comments:

Post a Comment