Saturday, August 23, 2014

MAUAJI YA ALBINO YANAVYOSABABISHA ATHARI KWA JAMII ONA KITUO HIKI WATOTO WANAVYOTESEKA

Hapa ni katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali cha Buhangija manispaa ya Shinyanga na hiki ni chumba cha wavulana, ambapo wamelazimika kuanza kulala kwenye jengo hilo kabla halijakamilika likiwa halina milango wala madirisha kutokana na kuwepo msongamano mkubwa wa watoto na kusababisha kulala kitanda kimoja watatu hadi wanne kutokana nsongamano uliopo, ambao umesababishwa na kuwepo mauaji ya watu wenye albinizim hapa nchini hususani mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi hivyo kituo hicho kutumika kulea walemavu hao wakiwemo wasioona,wasiosikia na Albino ambao ndiyo idadi kubwa wakitoka mikoa ya Simiyu,Geita,Mwanza,Tabora na Shinyanga.
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamu Hafidhi akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi misaada iliyotolewa na wadau kupitia shirika la Easy flex production la mjini Shinyanga.ambao walitoa chakula,mashuka na fimbo nyeupe za walemavu wasioona.
Mkurugenzi mtendaji wa Easy flex production Happness Kihama akisoma taarifa ya misaada waliyoitoa kwenye kituo hicho, kupitia harambee waliyoitisha ya kuchangia kituo cha Buhangija na kambi ya wazee Kolandoto vyote vya manispaa ya Shinyanga ambapo msaada uliotolewa unathamani ya sh milion 7,840,000.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buhangija na msimamizi wa kituo hicho akitoa maelezo kwa Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamu Hafidhi juu ya changamoto zilizopo ,alisema kwa sasa watoto wanalazimika kulala wanne kitanda kimoja kutokana na idadi kubwa ya watoto hasa Albino kufuatia kuanza kuibuka tena mauaji hayo mkoa wa Simiyu na Tabora wawili kujeruhiwa kwa kukatwa viungo vyao vya mwili.
Hili ni bweni la wasichana ambao hulala wanne kitanda kimoja hivyo kuwa na msongamano mkubwa licha ya wadau mbalimbali kusaidia kutoa misaada lakini bado haijakidhi mahitaji .
Meya akimkabidhi msimamizi wa kituo hicho mwalimu Peter Ajali, fimbo nyeupe 11 za watoto wasioona.
Mkama Shakengwa akiweka wazi mauaji ya albino yanavyotishia amani ya nchi kutoweka na kusababisha waishi kama wakimbizi nchini kwao na kuitaka serikali kutoa adhabu kali kwa wanaobainika kufanya unyama huo.

Mwenyekiti wa kamati inayosimamia upatikanaji wa misaada hiyo DKT.Ntoke akionyesha fimbo nyeupe zilizotolewa na Easy flex Production kwa ajili ya watoto wasioona.
Meya akikagua kisima cha maji cha kupampu kwa mkono akiwa na viongozi wa Easy flex .
Baadhi ya watoto wenye albinizim wanaosoma darasa la saba shule ya Buhangija Rehema Masunga na Doricas Sonda wakiishukuru Easy flex kwa msaada walioutoa .
Baadhi ya vyakula vilivyotolewa na wadau












No comments:

Post a Comment