Saturday, August 23, 2014

WAKIMBIZI 170 WAHOFIWA KUFA MAJI BAADA YA MASHUA ILIYOKUWA IMEWABEBA KUZAMA

Wakimbizi wakiondoka Libya kuelekea Ulaya
Mashua iliyobeba wakimbizi kama 170 ikielekea Ulaya, imezama mwambao wa Libya na inahofiwa watu wengi wamekufa.
Jeshi la wanamaji la Libya limewaokoa watu 17 na inawasaka abiria wengine.
Mashua hiyo ilikuwa na shida punde baada ya kuondoka bandari ya Qarabouli, mashariki ya mji mkuu, Tripoli.
Wavuvi waliwazindua wakuu ambao walituma waokozi.
Lakini afisa wa walinzi wa pwani wa Libya alisema kikosi chake hakina zana za kutosha, na mara nyingi wanahitaji kuazima mashua kufanya kazi hizo ya uokozi.
Na ndege imeshambulia maeneo ya wapiganaji Waislamu karibu na uwanja wa ndege wa Tripoli na kuuwa watu 10.
Ndege hiyo ililenga kambi ya jeshi kusini ya Tripoli, ambayo zamani ilikuwa makao makuu ya Muammar Gaddafi.
Hiyo ni mara ya pili kwa ndege kushambulia eneo hilo katika juma moja.
Jenerali anayepinga wapiganaji hao, Khalifa Haftar, alisema watu wake ndio waliofanya shambulio la mwanzo lakini wadadisi wanashuku kama ana uwezo huo.
Kikosi kimoja cha jeshi la wanahewa kimelaumu ndege kutoka nchi za nje.
  Via :BBC

No comments:

Post a Comment