Mkuu wa wilaya ya Bariadi Erato Sima ambaye ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilayani humo.
JESHI la polisi mkoani Simiyu limefanikiwa kuwakamata watu saba
wanaodhaniwa kuwa wauwaji wa aliyekuwa mlemavu wa ngozi (albino)
Munghu Mugata (40) aliyeuwawa kwa kukatwa mapanga mnamo mwezi mei huko
katika kijiji cha Gasuma kata mwaubingi wilayani bariadi.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Kudawa Yelema (52) ambaye ni mganga wa jadi,
Sitta Maduhu (39), Jasamila Sungwa (42), Mpamba Saguda (18), Dede Madono (54),
Majeshi Sunja (38), pamoja na Mabula Bindondo (52) wote wakulima na wakazi wa kijiji
cha Gasuma
Akiongea na waandishi wa habari ofisi kwake, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama mkoa ambaye pia ni mkuu wa mkoa Paschal Mabiti, alisema kuwa kati ya
watuhumiwa hao mmoja ni mganga wa jadi.
Alisema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na wasamalia wema, liliendesha
msako mkubwa wa kuwasaka wahusika wa tukio hilo, ambapo lilifanikiwa kuwatia
mbaroni watuhumiwa hao saba.
Alibainisha kuwa Dede Madono (54) mmoja kati ya watuhumiwa hao, aliugua ugonjwa
wa maralia wakati akiwa maabusu na kupelekwa katika hospitali ya Wilaya ya
Bariadi, ambapo alifariki dunia akiwa hospitalini hapo akipatiwa matibabu.
Mabiti alieleza jeshi la polisi bado linaendelea kumsaka mdhamini wa
mauaji hayo, pamoja na kutafuta sehemu viungo vya mlemavu huyo wapi vilipelekwa
ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani na kujibu tuhuma zinazowakabili.
Aidha mkuu huyo wa mkoa alieleza kuwa marehemu Lughata alimwacha mtoto wake
Tiri Kulwa (8) darasa la kwanza, ambaye alieleza kuwa kwa sasa mtoto huyo
anahudumiwa na halmashauri ya Wilaya ikiwemo kumsomesha.
Hata hivyo mkuu huyo alizitaka wilaya zote kuhakikisha wanakusanya
takwimu sahihi za watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwa pamoja na kutambua mahali
wanapoishi.
Alisema mbali na kuagiza kukusanya kwa takwimu hizo viongozi ngazi ya vijiji na
kata wameagizwa kuhakiksha albino wote wanawekewa ulinzi wa kutosha kwa
kushirikina na wanachi katika maeneo wanakoishi.
Sambamba na hilo mabiti alitoa onyo kali kwa watu wanatenda matukio hayo na
kuwataka kuacha mara moja, huku akieleza kwa atakayebainika kutenda unyama huo
utakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Tukio hilo lililotokea mei 12 mwaka huu katika kijiji ca Gasuma kata ya
mwaubingi Wilaya ya Bariadi Mkoani hapa, baada ya mlemavu wa ngozi Mugata
kuvamiwa na watu wasiojulikana majira ya saa 8 usiku akiwa amelala
nyumbani kwake. |
No comments:
Post a Comment