Mjumbe
wa bunge maalum la katiba kutoka kundi la 201,Thomas Magnus Mgoli
amelazwa katika hospitali ya mkoa Dodoma baada ya kupigwa na wanaodaiwa
kuwa 'vijana ambao mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA)'.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi akiwa kitandani kwake, Mgoli amesema
alishambuliwa na vijana hao jana usiku majira ya saa moja eneo la area D
anakoishi.
Amesema vijana
hao hukutana nao mara kwa mara anapokwenda dukani na huzungumzia
masuala ya bunge hilo, lakini hiyo jana walimshambulia kwa kumuambia
kuwa yeye ni CCM.
Pichani
waziri mkuu aliyejiuzulu na mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa
akimjulia hali Mh Mgoli hospitalini hapo, wote wako kamati moja.
via>>FikraPevu
No comments:
Post a Comment