MWANAFUNZI
aliyefahamika kwa jina la Athony John (14) mkazi wa kijiji cha Ihalo kata ya
Ilola tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga Mkoani hapa aliyekuwa
akisoma Darasa la tano katika Shule ya Msingi Ihalo amefariki Dunia wakati
akiogelea kwenye bwawa la Maji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Justus Kamugisha alisema tukio hilo
limetokea Agost 10 mwaka huu majira ya Saa tisa Jioni wakati mwanafunzi huyo
akiogelea kwenye bwawa la maji kuzama na kisha kusababisha kifo chake.
Kamugisha alisema kijana huyo akiwa
peke yake alikuwa anaogelea katika bwala la maji lenye kina kirefu ambapo
alishindwa kuongelea na kuanza kunywa maji hayo na kisha kuzama hadi kupelekea
kifo chake.
No comments:
Post a Comment