Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika,Godfrey Zambi amenusurika
kupata kipigo kutoka kwa wakulima wa zao la pamba katika kijiji cha
Marekano wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kwa madai ya kutoridhishwa na
majibu aliyoyatoa juu ya mbegu za pamba zisizo na manyoya(Quton)kutoota
katika musimu uliopita wa kilimo.
Tukio hilo limetokea kijijini hapo wakati Naibu Waziri
huyo alipofanya ziara ya kushitukiza ya kutembelea vituo vinavyonunua
zao hilo katika wilaya hiyo ili kukagua mizani zinayotumika kupimia zao
hilo kutoka kwa wakulima.
Wakati akitoa majibu kwa wakulima ambao walikusanyika ghafla wakati
akikagua Mizani hiyo katika moja ya kituo kilichopo kijijini hapo ambao
walihoji ni kwa nini serikali iliwalazimisha kununua mbegu hizo ambazo
hazikuota pamoja bei ya kununulia zao hilo.
VIA: Malunde blog-Na Samweli Mwanga-Simiyu
No comments:
Post a Comment