Monday, August 11, 2014

AJALI YA GARI YAUWA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU NA KUJERUHI WATATU.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha.
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Shinyanga  Dickson Jones(17)amefariki dunia baada ya gari alilokuwa anasafiria na wenzake baada ya kupinduka katika barabara ya Shinyanga kuelekea Maswa katika kijiji na kata ya Mwigumbi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kutokana na kile kilidaiwa kuwa mwendo kasi.

Kamanda Kamugisha amesema tukio hilo lilitokea jana saa moja usiku ambapo gari lenye namba za usajili T116 BDF aina ya Toyota mali ya Washi Construction ya Geita likiendeshwa na dereva ambaye jina lake halijafahamika  wala makazi yake likitoka Maswa kwenda Shinyanga lilipinduka na kusababisha kifo cha mwanafunzi huyo papo hapo.


Amewataja majeruhi kuwa ni  Kefa Japhet(20)ambaye ameuamia mguu wa kushoto na Hosea Japhet(18)aliyeumia mgongo, wote wanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Shinyanga na Ramadhani Mazuri(23) mkazi wa Kahama aliyeumia mkono na mguu wa kushoto na majeruhi wamelazwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga.



No comments:

Post a Comment