MBUNGE wa Maswa Magharibi, mkoani Simiyu John Shibuda (Chadema), amesema
hatagombea ubunge kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu ujao, kwa kuwa
amechoshwa na kauli za vitisho na kejeli dhidi yake, zinazotolewa na
baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho.
Amesema hayo jana kwa nyakati tofauti, wakati akizungumza na wazee wa
Mji wa Maswa na Malampaka wilayani humo, alipokuwa akijibu swali lao
kuhusu hatima yake ya kisiasa ndani ya Chadema, baada ya chama hicho
kutishia kumfukuza.
Alipoulizwa na wazee ni chama kipi atagombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu
ujao, alisema wakati ukifika atasema kwani kwa sasa bado anatimiza
wajibu wake wa kutetea wapiga kura wake ambao wengi wao ni wakulima na
wafugaji na yuko tayari kufukuzwa ndani ya Chadema kwa kuwatetea wao.
Alisema kuwa aliingia katika chama hicho kwa hiari yake baada ya kukataa
dhuluma alizodai kufanyiwa na CCM na kudhani ndani ya Chadema kuna
demokrasia na ukombozi wa kweli, lakini alichokikuta ni tofauti kwani
kila siku amekuwa akipata misukosuko kutoka ndani ya chama hicho.
"Mie niliingia Chadema kwa hiari yangu baada ya kuona dhuluma zilizokuwa
ndani ya CCM, chama kilichonilea kisiasa, nikaona heri niende Chadema
ambako nilidhani kuna demokrasia na ukombozi wa kweli, lakini
nilichokikuta humo ni tofauti kwani kila siku wazee wangu mnasikia
napata misukosuko isiyo na maana," alisema.
Alisema pamoja na misukosuko hiyo, amekuwa kimya muda mrefu kiasi kwamba
kuna wakati vijana ndani ya chama hicho walimtukana matusi, wakatoa
maneno mbalimbali ya kumdhalilisha kwa kumwita ‘Msaliti’ na ‘Pandikizi
wa CCM’, huku viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho, wakikaa kimya
bila kuchukua hatua.
"Pamoja na shutuma zote zinazotolewa juu yangu na kupachikwa majina
mbalimbali kuwa mie ni ‘Msaliti’ mara ni ‘Pandikizi la CCM’, lakini hata
siku moja sijawahi kuitwa katika Kamati Kuu ya Chadema na kuhojiwa
No comments:
Post a Comment