Tuesday, August 19, 2014

MWANDISHI WA HABARI WA KAMPUNI YA MWANANCHI ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi katika shirika la The Foundation for human healthy society(HUHESO Foundation) ambaye pia ni mwandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communications na mwenyekiti wa klab ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Shija Felician akizungumza na wanachama wa shirika hilo mara baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo katika kipindi cha miaka mitatu.


Wanachama wa shirika hilo wamemteua Felician kushika  nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu na kwamba bodi yake itakuwa na wajumbe kumi ambao watasimamia shughuli zote sanjari na kubuni mbinu mbalimbali za maendeleo ,ambapo bodi hiyo inaundwa na wataalamu mbalimbali kutoka sekta za serikali na binafsi.

Mkurugenzi  mtendaji wa Shirika hilo Juma Mwesigwa aliwataja viongozi wengine kwenye bodi hiyo kuwa , makamu mwenyekiti wa  bodi hiyo Avelina Ndakama pamoja na Atufigwege Mwakyaki ambaye atakuwa Mweka Hazina wa Bodi katika kipindi hicho cha miaka mitatu.


No comments:

Post a Comment