Wednesday, August 27, 2014

SHIRECU KUWAKOMBOA WAKULIMA WA PAMBA





ZAIDI ya kilo million  nane za pamba zinatarajiwa kununuliwa na chama kikuu cha ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) katika msimu wa mwaka
2014/2015,kutokana na baadhi ya makampuni ya kununua zao hilo kujitoa  kwa kudai kuwa soko la dunia limeshuka  hawatapata faida .


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga meneja wa SHIRECU mkoani hapa Joseph Mihangwa ,alisema mpaka sasa tayari wamenunua kilo million 4.8 za pamba katika vituo vyake vyote huku wakitarajia kufikisha kilo zaidi ya million nane  ili kufiki lengo walilokusudia.

Aisema mpaka sasa ni  asilimia 75 ya wakulima waliojitokeza kuuza pamba yao  huku asilimia 25 wakisubiri  kama soko litakuwa zuri ili wauze kwa bei itakayo kuwa na tija kwao kwani bei  iliyopo hivi sasa ni shilingi 750 kwa kilo moja.

‘ Soko la dunia  limekuwa baya  kwa kuangalia bei iliyopo  hata hii ya shilingi 750  tunayonunua  kutoka kwa mkulima  ni kubwa, hivyo tunanunua kwa matumaini huenda  soko la dunia bei yake ikawa nzuri baadaye ,kuna makampuni mengine yameacha ila sijajua ni sababu gani kuu lakini wanadai soko la dunia limeshuka”alisema.

Akizungumzia suala la mizani Mihangwa alisema hakuna changamoto  kwa upande wao kwani imekuwa ikisimamiwa na vyama vya msingi vya ushirika  kwa usahihi ambapo vilivyopo vyama ni  480 ,vilivyochini ya SHIRECU  ambapo kati ya hivyo  210 vimejiimarisha katika biashara na vilivyobaki vimeteteleka kutokana  uchumi wake  kutokuwa mzuri.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje akizungumzia zao hilo, alisema wakulima  wadogowadogo wamejitokeza kuuza ili kupata fedha na kukithi mahitaji ndani ya familia ambapo baadhi ya wakulima wakubwa wakisubiri soko kuwa zuri wakati msimu nao ukielekea mwisho.
Naye diwani wa kata ya Mondo  wilayani Kishapu mkoani linapolimwa zao hilo kwa wingi  John Ndama  ,alisema  wakulima wamekosa ujanja  imebidi wauze kwa bei hiyo na kwamba kuna kampuni ya   Villani ambayo ilianza kununua pamba kwenye baadhi ya maeneo kwa shilingi  800 kwa kilo moja .
Baadhi ya wakulima  wa  zao la pamba  mkoani Shinyanga  akiwemo  Maduhu Shija na Bernadetha  Joshua walisema  wakulima wamekubali kuuza kwa bei  ya shilingi 750 kwa kilo, kutokana na changamoto kubwa  ndani ya familia  kukosa kipato huku wakiunga mkono baadhi ya makampuni kujitoa  kwani wameona  wanapata  hasara.


No comments:

Post a Comment