Thursday, August 14, 2014

UHAMIAJI HARAMU NI TISHIO NCHINI MAAFISA WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO NA JINSI YA KUZIONDOA.

Maafisa uhamiaji kutoka mikoa ya kanda ya magharibi ya uhamiaji ambayo ni Simiyu,Geita,Mwanza,Tabora,Rukwa,Kigoma,Kagera,Shinyanga, Mara wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kujadili changamoto mbalimbali zinazokwamisha jitihada za kukabiliana na wahamiaji haramu nchini ikiwa ni pamoja na ukosefu wa boti ambazo zingetumika kufanya doria ziwa victoria na Ziwa Tanganyika, ili kuwakamata wahamiaji haramu wanaotumia njia za majini.
Naibu kamishina wa uhamiaji mkoa wa Shinyanga Annamaria Yondani akiwakaribisha maafisa uhamiaji kutoka mikoa mingine ambao walifika mkoani Shinyanga kwa ajili ya mkutano wa kanda ya magharibi wa uhamiaji.
Naibu kamishina wa uhamiaji mkoa wa Mwanza Remegius Pesambili ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya uhamiaji kanda ya magharibi,akisoma taarifa ya hali ya uhamiaji haramu na changamoto zake, ambapo alisema tatizo la uhamiaji haramu nchini limekuja na changamoto nyingi ambazo zinahatarisha usalama wa nchi ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa madawa ya kulevya,uvuvi haramu,uharibifu wa mazingira,uwindaji haramu mbuga za wanyama ,wizi wa magari na utakatishaji wa fedha haramu.
Mkutano unaendelea.

Maafisa uhamiaji wakiwa katika ukumbi wa Karena hotel tayari kwa ajili ya mkutano wa kanda ya magharibi.

Maafisa uhamiaji wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye  mkutano huo.
Katibu tawala msaidizi mkoa wa Shinyanga Projestus Rutabanzibwa akifungua mkutano wa maafisa uhamiaji kanda ya Magharibi mjini Shinyanga,ambapo alisisitiza idara ya uhamiaji kuendelea kutoa elimu kwa viongozi kuanzia vijiji hadi kata.
Waliosimama ni wawakilishi kutoka ofisi ya RPC mkoa wa Shinyanga,TAKUKURU na idara zingine.
Wakitafakari hotuba iliyotolewa na mgeni ramsi wakati akifungua mkutano.
Mkutano unaendelea.
Maafisa uhamiaji wakiwa katika picha ya pamoja













No comments:

Post a Comment