Wednesday, September 24, 2014

ASKOFU MKUU ALAANI WANAOUWA ALBINO NA VIKONGWE AWATAKA WATANZANIA KULIOMBEA TAIFA

ASKOFU mkuu wa kanisa la Tanzania Missionary Rivival Churh (TMRC) Jacob Lutubija akiwapaka mafuta na kuwaombea maaskofu sita mara baada ya kusimikwa katika kanisa la TMRC lililopo mtaa wa Ndembez
i manispaa ya Shinyanga ,maaskofu hao ni kutoka katika mikoa ya Morogoro, Mara,Dar es salaam, Geita ,Simiyu  na Mwanza .                                                                                                                                                     Katika ibaada ya kusimikwa maaskofu hao, Askofu mkuu Lutubija alitumia fursa hiyo kulaani na kukemea vikali kitendo cha watu wanaofanya ukatili wa kuwauwa na kuwanyofolea viungo vyao vya mwili  watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wakiamini watapata utajiri jambo ambalo si kweli na kuwataka kumrudia mungu na kuachana na mambo hayo ikiwamo mauaji ya vikongwe na matukio mengine ya ukatili.
Askofu mkuu wa kanisa la TMRC Jacob Lutubija akizungumza na waumini wa kanisa hilo mara baada ya ibaada kumalizika ,ambapo aliwaasa kuendelea kuliombea taifa kwani awali nchi haikuwa na matukio ya ajabu lakini sasa hali imebadilika vikiwemo vitendo vya ukatili na ufisadi.

Waumini wa kanisa la TMRC mtaa wa Ndembezi manispaa ya Shinyanga wakiwa kanisani.
                                
Maaskofu waliosimikwa wakisoma kiapo
Wanakwaya  wakitoa burudani wakati wa kusimikwa maaskofu



No comments:

Post a Comment