Thursday, September 4, 2014

BINTI WA MIAKA 19 AUAWA KIKATILI KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKIGONGA MLANGO

Binti wa miaka 19 auawa Detroit
Theodore Wafer
Jaji mmoja nchini Marekani amemhukumu mwanamume mmoja kifungo cha miaka kumi na saba jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua mwanamke mweusi ambaye hakua na silaha,
ambaye alikua akigonga mlango mkuu wa nyumba yake mapema asubuhi.

Theodore Wafer,ambaye ni mzungu, alijitetea kua alikua akihofia uhai wake ndipo akajitetea kwa kumpiga risasi binti huyo mweusi aliyekua na miaka 19, Renisha McBride mjini Detroit.

Jaji huyo alimkinza Theodore kwa maamuzi yake mabaya,lakini pia binti huyo hakustahili kufa.Binti Theodore alikua nagonga katika nyumba hiyo kuomba msaa baada ya kupata ajali ya gari.

Baada ya kufanyia uchunguzi mwili wa binti huyo walimkuta ana kiwango kikubwa cha pombe,mauaji ya binti huyo yalizusha maandamano, na kifo chake kinafananishwa na kijana Andrew kutoka Florida Trayvon Martin aliyepigwa risasi mwaka 2012.
 Via :BBC

No comments:

Post a Comment